Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miradi sita ya maji Meatu yaanza kutumia umeme

Tanki la kuhifadhi maji lilojengwa na Ruwasa katika Wilaya ya Meatu. Picha na Samwel Mwanga

Muktasari:

  • Vijiji vilivyonufaika na mabadiliko hayo ni pamoja na SangaItinje, Nkoma, Sakasaka, Ng’hoboko, Mwamalole na Mwangudo.

Meatu. Wakazi wa vijiji sita wilayani Meatu, mkoani Simiyu, wameanza kunufaika na huduma ya maji ya uhakika baada ya maboresho ya miradi ya maji iliyokuwa ikitumia nishati ya mafuta na sasa kuhamia kwenye matumizi ya umeme.

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi Aprili 17, 2025 na Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Emanuel Luswetura alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Mwanhunzi.

Mhandisi Luswetura amesema mabadiliko hayo yamelenga kupunguza gharama kubwa zilizokuwa zinatokana na matumizi ya mafuta na matengenezo ya mara kwa mara ya injini za dizeli zilizokuwa zikitumika kusukuma maji.

“Awali, uendeshaji wa pampu kwa kutumia mafuta ulikuwa na gharama kubwa, lakini sasa tumebadili mfumo na kutumia umeme wa gridi ya Taifa, jambo ambalo limepunguza sana gharama za uendeshaji,” amesema Luswetura.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kuboresha huduma za maji vijijini kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira.

Vijiji vilivyonufaika na maboresho hayo ni pamoja na Sangaitinje, Nkoma, Sakasaka, Ng’hoboko, Mwamalole na Mwangudo.

Yohana Jagadi, mkazi wa kijiji cha Sangaitinje, amesema kabla ya maboresho hayo, walilazimika kutembea zaidi ya kilomita tano kutafuta huduma ya maji, lakini kwa sasa yanapatikana karibu na makazi yao.

Nyumba ya kusukuma maji(Pump house)katika kijiji cha Sakasaka wilaya ya Meatu kilichowekewa nishati ya umeme. Picha na Samwel Mwanga

Naye Paulina Ntobi, mkazi wa Kijiji cha Sakasaka, amesema huduma ya maji kwa sasa ni ya uhakika na imesaidia wanawake kuokoa muda mwingi uliokuwa ukitumika kuyafuata.

Ruwasa kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), wamefanikiwa kufikisha umeme kwenye vituo vya miradi hiyo na kuweka miundombinu ya kisasa ya kusukuma maji.