Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikoa 25 kupata mvua kubwa kuanzia leo

Muktasari:

  • Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetabiri mvua kubwa kwa siku tatu kwenye mikoa 25, ikiwemo ya visiwa vya Unguja na Pemba.

Dar es Salaam. Kama unaishi kwenye mikoa hii 25 nchini chukua hatua kwa kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetabiri mvua kubwa itakayonyesha siku tatu kuanzia leo Machi 9, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 8, 2025, TMA imesema hali hiyo itashuhudiwa kwenye baadhi ya maeneo ya mikoa hiyo kati ya leo hadi Jumanne ya Machi 11.

Mikoa iliyopewa angalizo ni Kigoma, Katavi, Tabora, Singida, Dodoma, Simiyu, Mara, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Kagera, Geita, Mwanza na Shinyanga.

Mingine ni Tanga, Morogoro, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Mtwara, Lindi, Rukwa, Mbeya, Iringa, Songwe, Njombe na Ruvuma pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
"Kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani, baadhi ya makazi kuzungukwa na maji," imeandikwa kwenye taarifa hiyo.