Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfuko wa bima ya afya wa Mufti kusaidia wasiojiweza

Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa taasisi ya bima iliyoanzishwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, uliofanyika katika ukumbi wa makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) jijini Dar es Salaam jana. Picha na Said Powa.

Muktasari:

  • Waziri Mchengerwa amesema kuanzishwa kwa Mufti Bima Foundation ni mwendelezo wa jitihada za kuunga mkono hatua ya Serikali ya kuhakikisha Watanzania wanapata kinga ya bima ya afya.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesema hatua ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir kuanzisha Taasisi ya Mfuko wa Bima ya Afya ni miongoni mwa jitihada zitakazowezesha kuchochea maendeleo ya ustawi wa jamii.

Kwa mujibu wa Mchengerwa, tayari baadhi ya wananchi wameshaanza kunufaika na matunda ya mfuko huo unaolenga kusaidia upatikanaji wa bima ya afya kwa watu wasiojiweza pamoja na kutoa elimu ya bima kwa jamii.

Mchengerwa ameeleza hayo jana Alhamisi Mei 7, 2026 wakati akizundua mfuko huo katika ofisi za makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), jijini Dar es Salaam.

“Jambo hili linaonyesha dhamira njema ya kuwafikia wananchi katika huduma hii muhimu ya afya,” amesema Mchengerwa.

Baadhi ya masheikh na wadau wa sekta ya bima wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa taasisi ya bima ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir. Hafla hiyo imefanyika jana katika ukumbi wa makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) jijini Dar es Salaam. Picha na Said Powa.

Waziri huyo, amesema kuanzishwa kwa Mufti Bima Foundation ni mwendelezo wa jitihada za kuunga mkono hatua ya Serikali ya kuhakikisha Watanzania wanapata kinga ya bima ya afya.

Amesema tukio hilo, ni ishara ya mshikamano wa kitaifa na ushirikiano wa dhati kati ya Serikali na taasisi za dini, akieleza kuwa taasisi hizo zimeendelea kuwa mwanga mkubwa katika kuongoza wananchi kwenye misingi ya maadili, ustawi na mshikamano.

“Ushiriki wenu katika juhudi hizi, unaendelea kuwa nguzo muhimu katika safari ya kufikia Taifa lenye watu wenye afya bora na ulinzi wa kifedha dhidi ya gharama za matibabu,” amesema Mchengerewa.

Katika uzinduzi huo, Mchengerwa na familia yake walichangia Sh10 milioni huku akiahidi kutoa nyingine Sh30 milioni watakazochangishana yeye na wasaidizi wake wizarani.

Wakati Naibu Waziri wa Tamisemi anayeshughulikia sekta ya afya, Dk Rajab Seif amesema wizara hiyo itatoa ushirikiano wa kutosha katika mchakato huo, huku akiahidi kuchangia Sh20 milioni zitakazochangwa pia watumishi wa wizara hiyo.


Kuhusu Mufti Bima Foundation


Akizungumza kwa niaba ya Mufti, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kuu ya Bakwata, Sheikh Khamis Mataka amesema mfuko umejikita kuwasaidia wananchi wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu ili kuwezesha kupata huduma za matibabu.

Amesema mfuko ni muhimu kwa sababu kamati ya pamoja na viongozi wa dini mbalimbali ilifanya utafiti wa kubaini umasikini katika ngazi ya familia na kugundua familia milioni tatu, sawa na watu milioni 15 wapo katika changamoto.

“Tulibaini watu hao hawawezi kumudu gharama za matibabu wala kujinunulia bima ya afya. Kutokana na ukweli huu, nia ya mfuko huu ni kuchangia juhudi za Serikali za bima ya afya kwa wote,” amesema Sheikh Mataka.

Sheikh Mataka, amesema bima hiyo itazingatia taratibu za Kiislamu akimaanisha haikusudii kupata faida bali kile kinachopatika kinakwenda kuwasaidia wasiojiweza na wanaoshi katika mazingira magumu.

“Tutashirikiana na Serikali (Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini-Tasaf) kuwapata wahusika kuanzia ngazi ya chini kabisa hasa kwa kutumia mfumo wa Bakwata ambao upo kila eneo,” amesema Sheikh Mataka.

Sheikh Mataka amesema dhamira ya mfuko huo kukusanya nguvu ili kupunguza pengo la watu wasiojiweza ili kupata matibabu ya uhakika.