Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashine 64 za kamari zawaponza watatu

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga akionyesha aina ya mabonanza yaliyokamatwa yakifanya shughuli kinyume na utaratibu

Muktasari:

  • Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga amesema watuhumiwa watatu wamekamatwa katika operesheni maalumu iliyofanyika kuanzia Juni 5 hadi Juni 9, 2026 katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Momba na Mbozi.

Songwe. Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, limewakamata watu watatu kwa tuhuma za kuendesha michezo ya kubahatisha kinyume cha sheria na kukutwa na mashine 64 zisizoidhinishwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augustino Senga akizungumza leo Alhamisi Juni 11, 2026 ofisini kwake Mjini Songwe, amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika operesheni maalumu iliyofanyika kuanzia Juni 5 hadi Juni 9, 2026 katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Momba na Mbozi.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa ni Hashim Mahenge (30), mkazi wa Mpemba; Raymond Mbughi (34), mkazi wa Tunduma  na Steve Kyando (20), mkazi wa Mpemba.

Kwa mujibu wa Kamanda Senga, operesheni hiyo imebaini mashine 64 za michezo ya kubahatisha ambazo hazijathibitishwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania na zilikuwa zikitumika kuendesha michezo hiyo bila kufuata taratibu za kisheria.

Amesema uchunguzi zaidi uliofanyika nyumbani kwa Mahenge ulibaini uwepo wa karakana ndogo iliyokuwa ikitumika kutengeneza mashine hizo kinyume cha sheria.

Baadhi ya mabonanza yaliyokamatwa yakifanya shughuli kinyume na utaratibu

“Mahenge alikutwa na vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengeneza mashine hizo, ikiwemo hopper 13 za kuhifadhia na kutoa fedha kwenye mashine, display 32 za slot machines, monitor 10 za mashine hizo pamoja na vifaa vingine vya kielektroniki vinavyohusiana na utengenezaji wake,” amedai Kamanda Senga.

Amesema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutengeneza na kuendesha michezo ya kubahatisha kinyume cha sheria, kosa linalodaiwa kukiuka kifungu cha 81 cha Sheria ya Michezo ya Kubahatisha, Sura ya 41, marejeo ya mwaka 2023.

Kamanda Senga ametoa wito kwa wafanyabiashara kuacha kujihusisha na shughuli za michezo ya kubahatisha bila leseni na amewataka wanaoendesha shughuli hizo kinyume cha sheria kusitisha mara moja na kujisalimisha kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Pia, amewatahadharisha wananchi kuepuka kushiriki michezo hiyo wakati wa saa za kazi na badala yake kujikita katika shughuli za uzalishaji mali kwa ajili ya maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.

Operesheni hiyo imefanyika kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Omari Makame, alipofanya ziara Mei 12, 2026 katika Mji wa Mlowo, Wilaya ya Mbozi.

Katika ziara hiyo, mmoja wa wananchi aliwasilisha malalamiko akidai kuwa mashine zisizosajiliwa zinachangia mmomonyoko wa maadili miongoni mwa watoto na vijana, huku baadhi yao wakidaiwa kujihusisha na vitendo vya wizi wa fedha ili kushiriki michezo ya kamari.

Kutokana na malalamiko hayo, Makame aliliagiza Jeshi la Polisi na vyombo husika kufanya operesheni za kudhibiti uendeshaji usiofuata sheria wa michezo ya kuhatisha ili kulinda maadili ya watoto na vijana pamoja na kudumisha utulivu.