Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marufuku kuuza kahawa mbichi

Muktasari:

  • Mkuu wa wilaya hiyo, Shaabani Lissu aliwaambia waandishi wa habari kuwa, biashara ya obutura inasababisha wakulima wabakie kuwa maskini badala ya kuwaondolea hali hiyo.

Uongozi wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera umepiga marufuku biashara ya kuuza kahawa changa maarufu kwa jina la obotura, badala yake umewataka wakulima wauze yenye viwango vinavyotakiwa katika masoko makubwa ili wapate faida.

Mkuu wa wilaya hiyo, Shaabani Lissu aliwaambia waandishi wa habari kuwa, biashara ya obutura inasababisha wakulima wabakie kuwa maskini badala ya kuwaondolea hali hiyo. “Kuvuna kahawa ambayo haijakomaa kwa asilimia kubwa ni tamaa kwa wanaume wachache, niwatake maofisa ugani waendelee kutoa elimu kwa wakulima ili wabadilike,” alisema.

Mkulima Justus Philbert, mkazi wa Nyamilima, kata ya Mabira alisema sababu inayowafanya kuuza obutura ni kutokana na elimu ndogo waliyo nayo na wengine kukosa fedha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya familia zao.