Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mama mzazi wa Hayati Magufuli afariki dunia Chato

Mama mzazi wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Magufuli, Suzana Magufuli.

Muktasari:

  • Hayati Suzana Magufuli alikuwa akifahamika kama mlezi na nguzo muhimu ya familia ya Hayati Dk Magufuli, ambaye aliiongoza Tanzania kuanzia mwaka 2015 hadi 2021.

Mama mzazi wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Magufuli Suzana Magufuli, amefariki dunia leo Mei 25, 2026 nyumbani kwake Chato mkoani Geita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na mtoto wa Hayati Magufuli, Jesca Magufuli, leo Jumatatu Mei 25, 2026 akizungumza na AyoTV.

Jesca amesema Suzana Magufuli amefariki saa 1:00 usiku akiwa nyumbani kwake Chato.

“Bibi yetu (Suzana Mussa) amefariki saa moja usiku nyumbani kwake Chato baada ya kuugua kwa muda mrefu. Taratibu za msiba familia itawajulisha. Bwana ametoa na Bwana ametwaa,” amesema Jesca.

Hayati Suzana Magufuli alikuwa akifahamika kama mlezi na nguzo muhimu ya familia ya Hayati Dk Magufuli, ambaye aliiongoza Tanzania kuanzia mwaka 2015 hadi 2021.