Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makonda ataka wanaojenga kuwa na mpango wa kupanda miti

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda akizungumza leo Jumamosi Februari 15, 2025 katika  eneo la Shangarai,barabara kuu ya Moshi- Arusha, wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji miti na usafi kwa Mkoa wa Arusha.

Muktasari:

  • Akizungumza leo Jumamosi Februari 15,2025 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amezitaka mamlaka zinazohusika na utoaji wa vibali vya ujenzi, kutokuvitoa kwa mtu ambaye hataonyesha eneo atakayopanda miti katika eneo lake analojenga.

Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameagiza mamlaka zinazohusika na kutoa vibali vya ujenzi ikiwemo mipango miji, kutokutoa vibali vya ujenzi kwa mtu atakayeomba kibali bila kuonyesha eneo atakalopanda miti ili kupunguza athari za mazingira.

Ameagiza Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kila wanapojenga barabara kupanda miti ili kulinda mazingira.

Makonda ametoa maagizo hayo leo Jumamosi Februari 15,2025, akizindua upandaji miti mkoani hapa, katika eneo la Shangarai, Kata ya Ambureni, Barabara Kuu ya Moshi- Arusha.

Amesema ili kupambana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ni lazima kila anayeenda kuomba kibali cha ujenzi kuanzia sasa mkoani humo lazima aonyeshe anapopanda miti.

"Kuanzia leo kila anayeenda kuomba kibali cha ujenzi, lazima aonyeshe ujenzi anaofanya miti anapanda wapi hata kaka ni kiwanja cha mita za mraba 500,kama haupandi miti kwenye maombi yako ya ujenzi, wahusika wa utoaji wa kibali msitoe hicho kibali, Mipango miji, madiwani tumeelewana?

"Mnapoenda kukagua maendelezo ya ujenzi uwe mradi wa serikali au binafsi, nendeni na watu wa mazingira muangalie miti ilipopandwa. Watu wa mazingira mna taratibu za kufuatilia mtu anapoomba kibali cha ujenzi mfuatilie kama amepanda miti, tuwe na miti mingi na hali ya hewa nzuri,"

"Tarura na Tanroad msijenge barabara mkakata miti yote bila kupanda mingine, mnapojenga miradi ya barabara iwe mikubwa au midogo, lazima mpande miti, tutakuwa tunakagua kama tunavyokagua taa. Arusha ni mji wa kitalii, wageni wengi wanakuja haileti heshima wakaona mitaro michafu au makopo, tunapoteza heshima yetu," amesema

Kuhusu wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji, mkuu huyo amesema kutakuwa na shindani maalumu katika halmashauri za Jiji la Arusha, Meru na Halmashauri ya Arusha, shindano litakaloanza Machi 15,2025.

Amesema katika shindano hilo Mwenyekiti atakayesimamia usafi katika eneo lake atapewa zawadi ambapo mshindi wa kwanza atapewa Sh5 milioni,wa pili Sh3 milioni na wa tatu Sh2 milioni ambazo zitatolewa kama motisha kwao na watazipangia matumizi wenyewe.

"Tunatamani mwaka huu Arusha tuchukue namba moja kitaifa kwenye upandaji miti, usafi na tuboreshe mazingira yetu. Kwa upande wa mabalozi wa nyumba 10 nao watakaosimamia maeneo yao na kutoa elimu ya upande miti na kutunza mazingira," amesema

"Niwashukuru CRDB nimezungumza nao wamekubali Wenyeviti serikali za mitaa wanafanya kazi kubwa sana lakini mazingira yao ya kazi siyo mazuri sana hata kipato chao siyo kikubwa, kazi nyingi wanafanya kujitolea, angalia tuwatafutie fungu  la kuwatia moyo," ameongeza

"Kila mwezi mimi nitakuwa natoa Sh2 milioni kwa mshindi wa kwanza, wa pili Sh1 milioni na watatu Sh500,000. Zoezi hili tukafanye siyo kwa sababu ya hela ila kwa sababu tunajua athari za mabadiliko ya tabia nchi, mazingira ni uhai, ukiyaharibu yatakuadhibu," amesema

Meneja wa Benki ya CRDB, Kanda ya Kaskazini,  Cosmas Sadat, amesema benki hiyo inatekeleza kampeni ya Tanzania ya kijani kwa nchi nzima.

Kaimu Meneja wa Tanroad mkoa wa Arusha, Christopher Saul, amesema wataendelea kuhakikisha miti ya aina mbalimbali inapandwa katika barabara na kuisimamia.

Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sinoni, Anna Julius amesema kupitia kampeni mbalimbali wamepewa mafunzo ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira na kuwa inawasaidia kutunza mazingira na kuwa mabalozi wa mazingira katika jamii.