Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama Kuu yaamuru wadaiwa Exim wakamatwe

Muktasari:

  • Mahakama Kuu ya Tanzania (Divisheni ya Biashara) jijini Dar es Salaam,imeagiza kukamatwa kwa wadeni watatu wa Benki ya Exim Tanzania kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya kulipa deni lenye thamani ya Sh674.4 milioni na zaidi ya Dola 2 milioni za Marekani.

Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania (Divisheni ya Biashara) jijini Dar es Salaam,imeagiza kukamatwa kwa wadeni watatu wa Benki ya Exim Tanzania kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya kulipa deni lenye thamani ya Sh674.4 milioni na zaidi ya Dola 2 milioni za Marekani.

Kwa mujibu wa hati ya kukamatwa kwa wadeni hao iliyotolewa na mahakama hiyo katika kesi ya kibiashara nambari 95 ya mwaka 2015, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, ameagizwa na Mahakamana kuwakamata wadeni hao watatu ambao ni Chimanbhai Marghabai Patel, Pratik Chimanbhai Patel na Sonia Pratik Patel.

Hata hivyo, Kamanda Masejo alipozungumza na Mwananchi jana alisema hana taarifa juu ya hilo.

Kwa mujibu wa hati hiyo iliyosainiwa Septemba 13, 2021 na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, inasema watatu hao walihukumiwa Septemba 16, 2016 kuilipa

Benki ya Exim Tanzania Limited hata hivyo mpaka sasa fedha hizo hazijalipwa kwa benki hiyo.

Hivyo, imeelezwa kuwa kutokana na ucheleweshaji huo wa malipo, Mahakama imeamuru watu hao wakamatwe na wafikishwe mahakamani haraka iwezekanavyo.

“Unaagizwa kurudisha hati hii mnamo tarehe 27 Oktoba, 2021, sambamba na uthibitisho unao onyesha siku na namna ambavyo hati hii imetekelezwa au sababu zilizosababisha kushindwa kutekelezwa kwake,” inasomeka sehemu ya hati hiyo.