Mabango muhimu miradi ya barabara
Muktasari:
- Amesema kutokuwepo na taarifa zinazojitosheleza katika mabango ya miradi kunawafanya wananchi washindwe kuhoji matumizi halisi ya fedha zinazotumika.
Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa ili kuzuia rushwa katika miradi ya ujenzi wa barabara na majengo, mabango ya kutambulisha yanatakiwa kuonyesha gharama na muda wa kukamilika kwa miradi hiyo.
Amesema kutokuwepo na taarifa zinazojitosheleza katika mabango ya miradi kunawafanya wananchi washindwe kuhoji matumizi halisi ya fedha zinazotumika.
Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa ujenzi kuhusu uwazi na rushwa jana, Injinia Abdul Awadhi ambaye ni mshauri wa Mpango wa Uwazi wa Sekta ya Ujenzi (CoST), amesema kuwapo kwa uwazi kutasaidia kupunguza rushwa katika sekta ya ujenzi.
“Wananchi wanapojua gharama za miradi kupitia mabango hayo, wana uwezo wa kuhoji kama kuna thamani halisi ya fedha zinazotumika,” amesema.
Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwananchi au soma mtandaoni kupitia www.epaper.mcl.co.tz