Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ya Shetani wenzake yanguruma

Muktasari:

Kesi hizo ni ya ukusanyaji, usafirishaji na uuzaji vipande 118 vya meno ya tembo vyenye thamani ya zaidi ya Sh1.9 bilioni.

Dodoma. Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imeanza kuzisikiliza kesi za uhujumu uchumi, zinazomkabili mshtakiwa Boniface Malyango maarufu ‘Shetani hana huruma’ na wenzake wawili.

Kesi hizo ni ya ukusanyaji, usafirishaji na uuzaji vipande 118 vya meno ya tembo vyenye thamani ya zaidi ya Sh1.9 bilioni.

Washtakiwa wengine ni Malyango Abdallah, Ally Chaoga maarufu Babu na Lucas Malyango maarufu Lucas Mponze au Shimie, wote walikamatwa na maofisa wa kikosi kazi cha Taifa cha kupambana na ujangili.

Kesi hizo zinasikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Erick Fovo na Mwajuma Lukindo.

Mawakili wa Serikali, Paul Kadushi na Salim Msemo walidai kuwa katika kesi ya uhujumu namba 20 ya 2015, washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kujihusisha na nyara za Serikali kupitia genge la uhalifu.