Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Katibu mkuu UN asisitiza amani uchaguzi mkuu Tanzania

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres

Muktasari:

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres ametaka mchakato mzima wa uchaguzi nchini Tanzania kuwa huru na haki.

Dar es Salaam. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres ametaka mchakato mzima wa uchaguzi nchini Tanzania kuwa huru na haki.

Katika taarifa iliyotolea kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa Guterres amewataka viongozi wote wa kisiasa na wafuasi wao kushiriki shughuli ya uchaguzi  kwa amani na kujiepusha na vurugu.

Ametoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha kunakuwa na mazingira salama ambayo yataruhusu Watanzania kutumia haki yao ya kiraia ya kupiga kura.

Amesisitiza juu ya UN kuunga mkono juhudi za Tanzania  katika kuhakikisha kunakuwa na  maendeleo endelevu na kujenga mustakabali mzuri.

"Wakati Watanzania wanajiandaa kushiriki katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 28, natoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha kuwa upigaji kura unafanyika kwa umoja na kwa amani," amesema Guterress.