Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Katambi: Askari Polisi hustaafu majukumu, siyo kiapo

Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobasi Katambi.

Muktasari:

  • Waziri Katambi amesema hayo leo Alhamisi katika hafla ya kufunga mafunzo ya kozi namba 1/2025/ 2026 ya maofisa na wakaguzi wasaidizi wa Jeshi la Polisi iliyofanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi jijini Dar es Salaam yaliyohudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobasi Katambi amesema viapo vya askari wa Jeshi la Polisi havina ukomo, hivyo hata wakistaafu wanatakiwa kuishi navyo na si kwenda kinyume na kiapo walichokiapa.

Katambi amesema hayo leo Alhamisi, Mei 28, 2026 katika hafla ya kufunga mafunzo ya kozi ya maofisa na wakaguzi wasaidizi wa Jeshi la Polisi iliyofanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

"Mheshimiwa Rais (Samia) tukuahidi tutaendelea kusimamia suala la kiapo, lakini pia iwe ahadi yao kwao ya utii katika kufanya kazi hii kwa mujibu wa sheria na tukaendelee kuishi katika viapo vyetu.

"Tumeapa kwa Mungu, tumeapa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tumeapa kwa mamlaka ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Mheshimiwa Rais kiapo cha askari hakina ukomo, hata pale utakapostaafu, na kutoka nje ya majukumu viapo bado vipo hai," amesema Katambi.

Katambi amesisitiza askari polisi akistaafu huwa anastaafu majukumu tu na sio viapo hivyo amekumbusha kuzingatia suala ambalo ni jukumu la msingi kwao.

Amesema vyombo vya ulinzi na usalama vitaendelea kutekeleza majukumu yake kwa nidhamu na wale watakaokwenda kinyume na maadili watachukuliwa hatua na vitakuwa na utii kwa Amiri Jeshi Mkuu.

Mbali na hilo, Waziri Katambi amesema watahakikisha wakati wote vyombo vya ulinzi na usalama vinatenda haki, bila upendeleo wala kumuonea mtu.