Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kada wa CCM auawa kwa kupigwa risasi Kibiti

Muktasari:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema mauaji hayo yamefanyika usiku wa kuamkia leo (Jumapili)  katika Kijiji cha Nyambunda.

Kibiti. Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Bungu wilayani hapa, Alife Mtulia ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema mauaji hayo yamefanyika usiku wa kuamkia leo (Jumapili)  katika Kijiji cha Nyambunda.

Amesema Mtulia aliuawa na watu hao alipokuwa anakwenda kuoga.

Kamanda amesema mwili wa marehemu umepelekwa kituo cha afya cha Kibiti kwa uchunguzi.

Mauaji ya askari Polisi, viongozi wa Serikali za Mitaa na raia yamekuwa yakifanyika mara kwa mara katika wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani.

Jumanne wiki hii akiwasilisha bungeni bajeti ya wizara yake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba aliliambia Bunge kuwa Serikali itaanzisha mkoa mpya wa kipolisi katika wilaya za Kibiti, Rufiji, Mkuranga na Mafia. Utaitwa mkoa wa kipolisi Rufiji.