Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hatua kwa hatua maandamano waliokatwa majina ugawaji vizimba Kariakoo

Mwenyekiti wa CCM,  Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu, akiwasikiliza wafanyabiashara wa soko la Kariakoo walioandamana katika ofisi ndogo za CCM Lumumba kupinga kuondolewa kwa majina ya wanaotakiwa kurejea sokoni hapo

Dar es Salaam. Maandamano mengine ya wafanyabiashara yameibuka katika Soko la Kariakoo, jijini Dar es Salaam leo Julai 11, 2024 wakilalamikia majina yao kukatwa katika orodha ya wanaopaswa kurejeshwa sokoni humo.

Maandamano hayo yaliohusisha wafanyabiashara zaidi ya 800, yamelenga kuushinikiza uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo kuingiza majina yao ili nao wawe sehemu ya watakaopewa vizimba katika soko hilo, linalotarajiwa kuanza kutumika hivi karibuni.

Hilo linatokea zikiwa zimepita siku nne tangu mgomo na maandamano ya wafanyabiashara wa soko la Simu2000, Ubungo jijini humo kupinga kuhamishwa eneo hilo.

Msingi wa mgomo huo, ulikuwa ni kuishinikiza Manispaa ya Ubungo ifute uamuzi wake wa kukabidhi eneo linalotumiwa na Machinga kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) kwa ajili ya kujenga karakana.

Mgomo huo ulihitimishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kufika kuzungumza nao na kuahidi Jumamosi hii ya Julai 13, 2024 atafika hapo kutoa mrejesho wa suala hilo.

Kinachotokea kwa wafanyabiashara wa Karikakoo waliondolewa sokoni hapo Julai 2021, baada ya kutokea ajali ya moto iliyounguza soko hilo na kuathiri shughuli kadhaa, kimekuwa na mitizamo tofauti.

Julai 5, 2024, Mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo, Hawa Ghasia aliweka wazi watakaorejeshwa ni wale wenye mikataba na shirika pekee na wasiokuwa nayo wanapaswa kuomba kupitia mfumo rasmi.

Katika orodha hiyo uongozi wa soko hilo ulitoa orodha ya wafanyabiashara 891 kati ya 1,662 watakaorejea sokoni humo, huku wengine wakikosa vigezo vya kurejea.

Hata hivyo, uongozi huo ulishaweka wazi waliorejeshwa ni wale waliokuwa na mkataba na bodi ya uongozi huo, huku wale wasiokuwa nayo wanapaswa waombe kupitia mfumo rasmi.

Mariam Zuberi aliyefanya shughuli zake miaka 15 sokoni hapo, amesema majina mengi yaliyotoka watu hawayajui na kutaka suala hilo liangaliwe upya hata kwa kuwatumia viongozi wao, kwa kuwa ndio wanawajua.

Hata hivyo, hoja ya Mariam kwamba wengine waliorejeshwa hawafahamu, inataka kufanana na kauli aliyoitoa aliyekuwa Meya wa Kinondoni baadaye Ubungo, Boniface Jacob aliyeitoa juu ya mgomo wa wafanyabiashara wa Simu2000.

Jacob maarufu Boni Yai alisema baadhi ya maeneo kwenye soko hilo la Simu2000 walijigawia viongozi kisha nao wakapangisha.

Anachokieleza Jacob kiliwahi kujitokeza katika Soko la Machinga Complex, Dar es Salaam na baadhi ya maeneo mengine ya biashara kwa mtu mmoja kuweza kuwa na visimba hata 20 kisha naye anawapamngisha wafanyabiashara.

“Unajua kinachotokea hapo Kariakoo, unaweza kukutna mtu mmoja ana visimba hata 50, naye anakodisha na ndicho kinaweza kuwa kimejitokeza na ndio maana wengi hawajarudi kwani hawakuwa na mikataba na soko hilo,” amesema mmoja wa viongozi wa halmashauri ya Ilala aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Mei 22, 2024, Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Mafinga, wilayani Mufindi, Mkoa wa Iringa walisalimu amri na kukubali kusaini mikataba ya kukodi vibanda 331 vinavyomilikiwa na Serikali, baada ya kuwepo tishio la kuvibomoa.

Ni baada ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba kuagiza ufungwe utepe kuzunguka vibanda hivyo, akitaka vibomolewe kutokana na mvutano uliokuwepo.

Mgogoro baina ya Serikali na wafanyabiashara hao, umedumu kwa miaka tisa wakishindwa kukubaliana, walipoketi meza moja na Serukamba kusaka suluhu.

Chanzo cha yote ni kuwataka wafanyabiashara hao kulipa kodi ya Sh80,000 kwa mwezi kutoka Sh9000.

Taarifa zilizokuwapo, ni kwamba wafanyabiashara hao walikuwa wakilip[a halmashauri Sh90,000 huku wao wakijipatia kiasi kingine kulinagana na makubaliano na wale walioo wapangisha.

Mgomo ulivyokuwa

Katika mgomo wa leo, ulianza kwa wafanyabiashara hao kujikusanya katika Viwanja vya Mnazi Mmoja asubuhi kwa ajili ya kujiandikisha kwa maofisa wa Shirika la Masoko la Kariakoo, shughuli iliyoanza tangu saa 2:00 asubuhi.

Kabla shughuli hiyo haijaisha, sauti za malalamiko ya wafanyabiashara wakionyesha kuchoshwa na utaratibu wa kuhakikiwa.

Baadaye, walikusanya viti na meza walizotumia maofisa hao na kuwafanya watumishi hao waondoke viwanjani hapo.

Wakati maofisa hao wanaondoka, baadhi ya wafanyabiashara nao walianza safari ya kuendelea zilipo ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi (CCM) Lumumba, waliandamana hadi eneo hilo.

Nyimbo za ‘tunataka haki yetu, tunataka soko letu’ ndizo zilizokuwa zikisikika kutoka kwa wafanyabiashara hao.

Dakika chache baadaye walifika katika ofisi hizo na kupokelewa na maofisa wa CCM, akiwemo Mkuu wa Utawala wa chama hicho, Marco Mbaga aliyewataka watulie kwa kuwa tayari uongozi wa Serikali Wilaya umeshaarifiwa.

Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu naye alizungumza na wafanyabiashara hao akisisitiza msimamo wa Serikali ni kuhakikisha wote wanarejea sokoni.

Baada ya kelele na vuguvugu la maandamano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo alifika katika ofisi hizo saa 6:00 mchana, akiahidi kuwakutanisha na Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila kesho Ijumaa.

"Niwahakikishie hakuna mtu atakayepoteza haki yake katika hili, kesho asubuhi saa mbili tukutane kwa kwa Mkuu wa Mkoa," alisema.

Kauli hiyo ndio uliokuwa mwisho wa maandamano hayo.