Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

DPP amkatia rufaa Dk Slaa Mahakama ya Rufani

Dk Wilbrod Slaa akisalimiana na Mwenyekiti wa Chadema, Wakili Tundu Lissu katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu Dar es Salaam kabla ya kusomewa uamuzi wa mashauri yake mawili yaliyotokana na kesi ya Jinai inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Muktasari:

  • DPP amewasilisha kusudio la rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu dhamana ya Dk Willibrod Slaa, anayekabiliwa na shtaka la kusambaza taarifa za uongo mtandaoni.

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) amewasilisha kusudio la kukata rufaa kupinga uamuzi uliyotolewa na Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam dhidi ya Mwanasiasa Mkongwe nchini Tanzania, Dk Willibrod Slaa.

Uamuzi wa Mahakama Kuu jana, uliielekeza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kushughulikia suala la dhamana ya mwanasiasa huyo na kutoa uamuzi wa pingamizi la uhalali wa kesi ya jinai inayomkabili mahakamani hapo kwa haraka.

Kufuatia uamuzi huo, DPP amewasilisha notisi ya kukata rufaa jana Januari 30, 2025 katika Mahakama ya Rufaa.

Hayo yamefahamika leo Ijumaa Januari 31, 2025katika Mahakama ya Kisutu baada ya pande mbili za keshi hiyo kuitwa kwa ajili ya “kusikiliza maelekezo ya Mahakama”.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema ameieleza Mahakama ya Kisutu jkuwa: "Mheshimiwa hakimu, kwa mujibu wa kumbukumbu za mahakama, kesi hii ilipangwa kusikilizwa Februari 6, 2025 katika Mahakama hii lakini leo ni Januari 31, 2025, tumeitikia wito kwa sababu na sisi tumeitwa na mahakama yako kwa ajili ya kusikiliza maelekezo yako, hivyo tupo tayari kusikiliza" amesema Wakili Mrema mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.

Ametoa taarifa pia kwamba upande wa Jamhuri umekwishawasilisha notisi ya kukata rufaa Mahakama ya Rufani.

Amedai kutokana na kuwasilisha notisi hiyo, wanaomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu isitoe uamuzi wowote katika kesi ya msingi, mpaka rufaa iliyowasilishwa Mahakama ya Rufani itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Maelezo ya Mrema yamepingwa na mawakili wanane wanaomtetea Dk Slaa wakiongozwa na Hekima Mwasipu na Peter Madeleka.

Jopo la mawakili wanane wanaomtetea Mwanasiasa mkongwe nchini, Dk Wilbrod Slaa, wakijadiliana jambo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Picha na Hadija Jumanne

Mwasipu amesema wameitwa Mahakama hapo kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa pingamizi la dhamana na wapo tayari kusikiliza.

Pia amehoji sababu za mshtakiwa kutofikishwa mahakamani hapo, hoja ambayo ilijibiwa na upande wa mashtaka kuwa mahabusu wote hawakuletwa kutokana na changamoto ya usafiri wa gari la Magereza.

Kutokana na hali hiyo, hakimu Beda ameahirisha kwa muda wa saa mbili kesi hiyo, ili aweze kupitia baadhi ya sheria kabla ya kutoa uamuzi wa kuendelea na kesi au kutokuendelea.

Jana Januari 30, 2025 Mahakama Kuu iliielekeza Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dar es Salaam kushughulikia suala la dhamana ya mwanasiasa huyo na kutoa uamuzi wa pingamizi la uhalali wa kesi ya jinai inayomkabili mahakamani hapo kwa haraka.

Mbali na maelekezo hayo kwa mahakama ya Kisutu, pia kupitia sakata la dhamana ya mwanasiasa huyo, Mahakama Kuu ilitoa maelekezo maalumu kwa mahakama zote za chini namna ya kushughulikia suala dhamana za washtakiwa wa kesi za jinai.

Katika maelekezo hayo, imezitaka mahakama hizo za chini yake kuweka kipaumbele cha kwanza kabisa kushughulikia dhamana kuliko masuala yoyote yanayohusiana na kesi hizo, huku ikisisitiza kuwa duala la dhamana linapaswa lishughulikiwe siku ya kwanza kabisa mshtakiwa anaposomewa mashtaka.

Dk Slaa alifungua mashauri hayo kutokana na mwenendo wa kesi ya jinai inayomkabili katika Mahakama ya Kisutu, akiiomba Mahakama Kuu iitishe na kupitia mwenendo wa shauri dogo lililofunguliwa na Jamhuri kupinga dhamana yake na wa kesi ya msingi, kujiridhisha na usahihi na uhalali wake.

Mashauri hayo yote yalisikilizwa na Jaji Kirekiano moja Alhamisi na lingine Ijumaa iliyopita.

Dk Slaa anakabiliwa na shtaka moja la kusambaza taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii ya X, zamani ikijulikana kama Twitter.


Endelea kufuatili mitando yetu