Dk Mpango ahimiza elimu ya lishe bora kwa wananchi

Muktasari:
- Dk Mipango ameyasema hayo leo Jumapili Januari 29, 2023 katika ibada ya kumsimika Askofu Philipo Mafuja kuwa Askofu wa Kanisa la Afrika Inland Church Tanzania(AICT) Dayosisi ya Pwani.
Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ameomba viongozi wa dini kutoa elimu ya umuhimu wa lishe bora kwa waumini wao kwa kuwa hali sio nzuri.
Dk Mipango ameyasema hayo leo Jumapili Januari 29, 2021 katika ibada ya kumsimika Askofu Philipo Mafuja kuwa Askofu wa Kanisa la Afrika Inland Church Tanzania(AICT) Dayosisi ya Pwani.
Amesema lishe hasa kwa wajawazito na watoto sio nzuri, ‘’naomba muwakumbushe waumini wetu umuhimu wa lishe bora haswa katika kipindi cha kwanza cha ujauzito hadi mtoto anapofikisha miaka mitatu tangu alipozaliwa.’’
“Tuchukue hatua za makusudi kuhakikisha watoto wetu wanapata lishe bora kwa Taifa bora lijalo kwani hata Askofu asingepata lishe bora leo asingekuwa na nguvu ya kutangaza neno la injili.’’
Dk Mpango pia alihimiza utunzaji mazingira kwa kukemea ukataji ovyo wa misitu na kuhamasiha upandaji wa miti hasa katika msimu huu wa mvua.