Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

China na Tanzania kushirikiana uzalishaji wa nishati jadidifu

Muktasari:

  • Ziara ya Makamba imezaa matunda baada ya nchi hiyo kutoa fursa ya mafunzo kwa watalaamu wa Kitanzania.

Dar es Salaam. Ziara ya Waziri wa Nishati, January Makamba nchini China imezaa matunda baada ya nchi hiyo kuahidi kushirikiana na Tanzania katika uzalishaji wa nishati jadidifu chini ya mpango wa Belt and Road Energy Partnership.

Kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi hizo, China imeahidi kutoa fursa za mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa Tanzania katika ubunifu na uzalishaji wa teknolojia za uzalishaji wa nishati na kushirikiana katika utafutaji na uendelezaji wa miradi ya nishati ya gesi asilia jambo linalotiliwa mkazo na Rais Samia Suluhu.

Katika ziara hiyo Waziri Makamba alikagua baadhi ya mitambo ya kufua umeme katika Bwawa la Julius Nyerere inayozalishwa nchini China katika Kiwanda cha Kampuni ya Dong Fang Global jijini Sichuan.