CCM yawafuatilia viongozi wake wanaopotosha umma

Muktasari:
- Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimesema kinafutilia kwa makini mienendo ya baadhi viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha umma na kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Samia Suluhu na maadili ya chama.
Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimesema kinafutilia kwa makini mienendo ya baadhi viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha umma na kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais Samia Suluhu na maadili ya chama.
Taarifa iliyotolewa leo na CCM, Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka inawakikishia wanachama na Watanzania kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote ambao wanatumia nafasi iyo kusukuma ajenda zao binafsi, kwa mujibu wa Katiba, kanuni za maadili na uongozi za CCM