CCM wamuomba radhi Samia

Muktasari:
- Katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amemuomba radhi mwenyekiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan kwa kunukuliwa vibaya katika gazeti la Uhuru linalomilikiwa na chama hicho wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha BBC juzi.
Dar es Salaam. Katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amemuomba radhi mwenyekiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan kwa kunukuliwa vibaya katika gazeti la Uhuru linalomilikiwa na chama hicho wakati akihojiwa na kituo cha runinga cha BBC juzi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Agosti 11, 2021, Chongolo amesema maneno hayo ni ' sina wazo la kuwania urais 2025- Samia', akieleza kuwa hayakutamkwa na kiongozi mkuu huyo wa nchi.
"Amelishwa maneno na uungwa ni vitendo sisi ni waungana tunamuomba radhi Rais Samia. Hakuzungumza maneno yaliyoandikwa kwenye gazeti la leo la Uhuru, " amesema Chongolo.