Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Boti ya Sh4 bilioni kuimarisha uokoaji Ziwa Victoria

Boti maalumu ya kisasa ya uokoaji na huduma za matibabu ikiwa kwenye lori kwa ajili ya kuisafirisha kutoka bandari ya Mtwara kwenda mkoani Mwanza. Picha na Frank Saidi

Muktasari:

  • Boti hiyo ni moja kati ya tatu ambazo mataifa yanayoshjirikiana Ziwa Victoria – Tanzania, Kenya na Uganda yalikubalina kununua ili kukabiliana na changamoto ya ajali ziwani humo.

Mtwara. Katika jitihada za kupunguza vifo vya wavuvi vinavyotokana na ajali za mara kwa mara katika Ziwa Victoria, Serikali ya Tanzania imepokea boti maalumu ya kisasa ya uokoaji na huduma za matibabu yenye thamani ya Sh4 bilioni.

Boti hiyo, ambayo ni sehemu ya makubaliano ya kikanda kati ya Tanzania, Kenya na Uganda, inalenga kuimarisha uwezo wa ufuatiliaji na uokoaji ndani ya ziwa hilo ambalo hupoteza maisha ya zaidi ya wavuvi 5,000 kila mwaka.

Kutokana changamoto hiyo, Serikali za nchi hizo zinazotumia ziwa hilo, zilikubaliana kununua boti zitakazosaidia kufanya ufuatiliaji na uokoaji katika Ziwa Victoria.

Hayo yamebainishwa Aprili 11, 2025 na Meneja wa usajili na ukaguzi wa meli wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (Tasac), Saidi Kaheneko wakati wa upokeaji wa boti hiyo katika Bandari ya Mtwara kutoka Uturuki ilikotengenezwa.

Amesema boti hiyo ni moja kati ya tatu ambazo wamekubalina kununua ili kukabiliana na changamoto ya ajali ziwani.

“Ndani ya mwaka mmoja ndani ya Ziwa Victoria, vinatokea vifo takribani 5,000 vya wavuvi ndani ya maji na si kwa upande wa Tanzania pekee, ni pamoja na Kenya na Uganda.

Lori likiwa limebeba boti maalumu ya kisasa ya uokoaji na huduma za matibabu kwa ajili ya kuisafirisha kutoka bandari ya Mtwara kwenda mkoani Mwanza. Picha na Frank Saidi

“Marais wa nchi zote tatu walikaa wakaangalia namna ya kupunguza vifo kwa upande wa Tanzania, tumekubali kununua boti tatu na kujenga jengo la ufuatiliaji linalojengwa Mwanza,” amesema.

Ameongeza kuwa huo ni mradi wa kikanda, walikubaliana nchi tatu lakini baadaye Kenya ilijitoa, zikabaki Tanzania na Uganda kutekeleza makubaliano hayo.

Amesema Tanzania itanunua boti tatu, moja ndiyo hiyo iliyofika na mbili zimekamilika, ila waataalamu wataenda Uturuki kuzikagua, wakiona zinakidhi viwango walivyokubaliana, zitakuja.

“Hizo boti nyingine zitakuja ndani ya mwezi mmoja na nusu kama wataalamu wetu watakuta zimekidhi viwango,” amesema.


Kusafirishwa kwa barabara

Boti hiyo ya kubebea wagonjwa itasafirishwa kwa njia ya barabara kutoka Mtwara kupitia Songea hadi Mwanza.

Meneja huyo amefafanua kuwa boti hiyo imeshushwa kwenye bandari hiyo kwa sababu ina uzito mkubwa, hivyo ilitakiwa ipatikane meli yenye uwezo wa kuibeba na iliyopatikana ilikuwa inaenda Mtwara.

 “Boti hii ina uwezo wa kuchukua wagonjwa 16 kwa wakati mmoja na ina vyumba viwili kwa ajili ya wagonjwa wa dharura.

Ameongeza kuwa boti hiyo ina vyumba viwili kwa ajili ya wagonjwa wa dharura na ina vifaa vyote vinavyohitajika kwa wagonjwa wa dharura vitakavyowawezesha kupatiwa matibabu wakiwa kwenye boti hiyo.

“Boti hii ina vyumba viwili vya wagonjwa wa dharura (ICU), kimoja ni kwa ajili ya wanaume na kingine ni kwa ajili ya wanawake, pia, kuna vitanda viwili kwa ajili ya wagonjwa wasio wa dharura na ina eneo la chini na juu,” amesema.

Meneja Uhusiano na Masoko (Tasac), Saidi Mkabakuli amesema ujio waboti hiyo unaenda kuwa faraja kwa wakazi wa maeneo ya Ziwa Victoria.

“Boti hii itaenda kuwa faraja kwa wakazi wa maeneo ya Ziwa Victoria kwa sababu ikitokea dharura, itawasaidia kwenye uokoaji na kuwapatia matibabu,” amesema Mkabakuli.