Bibi, mjukuu wauawa
Muktasari:
- Bibi na mjukuu wake wameuawa kwa kukatwakatwa na mapanga, kwenye Kijiji Cha Ibambangulu,kata ya Mwatunduwilayani Nzega.
Tabora. Bibi na mjukuu wake wameuawa kwa kukatwakatwa na mapanga, kwenye Kijiji Cha Ibambangulu,kata ya Mwatunduwilayani Nzega.
Diwani wa kata hiyo, Paachal Lugonda amesema tukio hilo limetokea usiku mwishoni mwa wiki.
Akielezea tukio hilo amesema bibi aitwaye Nyamizi Ngassa na mjukuu wake walikatwa mapanga baada ya kuvamiwa usiku wakiwa wamelala na kusababisha vifo vyao.
Katika tukio hilo amesema mjukuu mwingine wa marehemu, alinusurika baada ya kufanikiwa kukimbia na kwenda kujificha na sasa amehifadhiwa sehemu kwa usalama wake.
"Tayari Polisi wanaendelea na uchunguzi wao ili kujua chanzo Cha mauaji hayo,"amesema.
Ofisa tarafa ya Nyasa, Elikado Komanya ameeleza kuwa mauaji hayo ni mwendelezo wa matukio ya mauaji katika siku za karibuni na kutaka wananchi wabadilike na kuachana na mauaji.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Safia Jongo,hakuweza kupatikana kuelezea tukio hilo..