Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

135,027 waomba ajira TRA, kuajiriwa kabla ya Juni

Kamishna  Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda akizungumzia mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita

Muktasari:

  • Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema watu 135,027 wameomba kuajiriwa katika nafasi 1,596 zilizotangazwa Februari mwaka 2025.

Dodoma. Watu 135,027 wameomba ajira katika nafasi 1,596 zilizotangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Februari 6, mwaka 2025 TRA ilitangaza nafasi za ajira katika idara za mapato ya ndani, forodha na ushuru, usimamizi na utawala wa raslimali watu.

Nyingine ni utafiti na mipango, fedha, ukaguzi wa ndani, mambo ya ndani na idara ya viatarishi na uzingatiaji.

Hayo yamesemwa leo Machi 12, 2025 na Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda wakati akielezea mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita na mwelekeo wa mamlaka hiyo.

Amesema mwitikio wa kufanya kazi TRA umekuwa mkubwa akitolea mfano kuwa  wametangaza kazi 1,596, lakini hadi wanakamilisha siku ya mwisho ya kupokea maombi walioomba walikuwa ni 135,027.

Amesema wiki ijayo mkurugenzi wa utawala atatoa utaratibu utakaofuatia kuhusiana na ajira hizo.

“Nataka niwahakikishie Watanzania tunataka ‘best brain’ zije TRA ili weledi uendelee kuimarika. Tutaweka mazingira ya haki na usawa ili kila mtu mwenye sifa apate fursa na ajira ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania,”amesema.

Amesema mamlaka hiyo imefanikiwa kuongeza watumishi kutoka 4,749 kabla ya Machi 2021 hadi 6,989 kufikia Machi 2025.

Amefafanua kuwa ongezeko hilo ni sawa na nyongeza ya watumishi 2,240, sawa na asilimia 47.

Amesema katika kipindi cha miaka minne, imechukulia hatua wachache waliokwenda kinyume na maadili ikiwemo kuwafukuzwa kazi  watumishi 14.

Amesema mbali na hilo kuna watumishi sita wameshushiwa mshahara, sita wameshushwa vyeo, 12 wameshushwa vyeo na kupunguziwa mshahara na 22 wamepewa onyo la maandishi.

Aidha, Mwenda amesema katika kipindi cha miezi minane kuanzia  Julai 2024 mpaka Februari 2025, TRA imefanikiwa kukusanya Sh21.20 trilioni  sawa na ufanisi wa asilimia 104, ya lengo la kukusanya Sh20.42 trilioni ambao ni ukuaji wa asilimia 17 ukilinganisha na Sh18.06 trilioni iliyokusanywa kipindi kama hicho mwaka 2023/24.

Amesema katika kipindi cha miaka minne ya Samia makusanyo ya kodi yanayokusanywa na TRA yameongezeka kwa asilimia 78, kutoka Sh11.92 trilioni hadi Sh21.20 trilioni.

Mwenda amesema katika kipindi cha miezi minane ya Julai, 2020, mpaka Februari, 2021, marejesho ya kodi kwa wafanyabiashara yalikuwa ni Sh92,372 milioni, wakati miaka minne baadaye katika kipindi cha Julai 2024, hadi Februari, marejesho ni Sh1.2 trilioni.

Pia amesema wamejenga mifumo ya Tehama katika usimamizi wa kodi ujenzi na uboreshaji wa mifumo ya TRA .