Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shirika la Bandari Zanzibar lakusanya Sh3.6 bilioni kwa mwezi

Shirika la Bandari Zanzibar lakusanya Sh3.6 bilioni kwa mwezi

Muktasari:

  • Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) limekusanya Sh3.6 bilioni mwezi Machi, 2021.

Unguja. Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) limekusanya Sh3.6 bilioni mwezi Machi, 2021.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Aprili 20, 2021 na mkurugenzi wa shirika hilo, Nahaat Mohamed Mahfoudh wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,  Hemed Abdulla ofisini kwake.

“Shirika limepata mafanikio makubwa kwa muda mchache, mfano makusanyo ya mwezi Machi yamefikia Sh3.6 bilioni huku faida ikiwa ni Sh2.2 bilioni,” amesema.

Abdulla ametumia fursa hiyo kuwataka watendaji wa umma kuwajibika hususani katika kusimamia makusanyo ya fedha zitakazosaidia kujenga miradi mikubwa ya maendeleo.

Naye Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Rahma Kassim Ali amesema wizara kwa kushirikiana na shirika hilo wamejitahidi kutatua changamoto mbalimbali ili kuhakikisha kila jambo linakwenda kama lilivyopangwa.