Papa ateua Balozi wa Vatican Tanzania

Muktasari:
- Papa Francisko amemteua Askofu Mkuu Angelo Accattino kuwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania.
Dar es Salaam. Papa Francisko amemteua Askofu Mkuu Angelo Accattino kuwa Balozi wa Vatican nchini Tanzania.
Kabla ya uteuzi huo, Accattino alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Bolivia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Askofu Mkuu, Accattino alizaliwa Julai 31, 1966, nchini Italia.
Baadaye Juni 25, 1994 alipewa daraja la upadre na kuanza utume wake katika masuala ya diplomasia ya Vatican, Julai 1, 1999.
Ilipofika Septemba 12, 2017 Papa Francisko alimtua kuwa balozi wa Vatican nchini Bolivia na kumpandisha hadhi kuwa Askofu Mkuu na kuwekwa wakfu kama Askofu mkuu Novemba 25, 2017.