Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mossad walivyodukua kamera za barabarani, kumuua Khamenei

Muktasari:

  • Mashambulizi kati ya Marekani, Israel na Iran yaendelea; vifo 787 vyaripotiwa Iran, balozi zafungwa Mashariki ya Kati, masoko ya fedha yadidimia huku hofu ya nishati na vita kupanuka ikiongezeka.

Dar es Salaam. Mashambulizi ya anga Mashariki ya Kati yameingia siku ya nne leo huku milipuko mikubwa ikitikisa miji ya Tehran, Iran na Beirut, Lebanon huku masoko ya fedha duniani yakishuka na hofu ya kuvurugika kwa usambazaji wa nishati kufuatia vita vya anga kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Ripoti mpya zimeibua madai mazito kuwa maofisa wa ujasusi wa Israel (Mossad) walidukua mtandao wa kamera za barabarani jijini Tehran kwa miaka kadhaa, wakifuatilia mienendo ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei, walinzi wake na maofisa wengine waandamizi kabla ya kuuawa kwake katika shambulio la anga mwishoni mwa wiki.

Wakati hayo yakiendelea, mamlaka za Iran zimesema hadi sasa watu 787 wamepoteza maisha kufuatia mashambulizi yanayofanywa na Marekani na Israel katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo huku nayo ikijibu mapigo kwa kuzishambulia, pamoja na washirika wake.

Moshi ukiwa umetanda angani katika moja ya maeneo Tehran. Picha na Mtandao

Ndege zisizo na rubani za Iran zimeshambulia ubalozi wa Marekani nchini Saudi Arabia na kusababisha uharibifu mdogo pamoja na moto, baada ya awali kulenga ofisi ya ubalozi huo nchini Kuwait.

Kufuatia mashambulizi hayo, Marekani imefunga balozi zake katika mataifa hayo na kuamuru wafanyakazi wa Serikali wasio wa lazima pamoja na familia zao kuondoka katika nchi kadhaa za Mashariki ya Kati.

Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kutoa majibu kwamba vita hiyo haina kikomo, walipoulizwa vita hivyo vingedumu kwa muda gani.

Chanzo kilichozungumza na Shirika la Habari la Reuters kimesema kampeni ya kijeshi ya Israel ilikuwa imepangwa kudumu kwa wiki mbili, lakini inaendelea kwa kasi zaidi ya ilivyotarajiwa.

Kwa mujibu wa chanzo hicho kinachofahamu mpango wa vita wa Israel, lengo kuu ni kuiondoa madarakani Serikali ya viongozi wa kidini wa Iran, bila kuwepo muda maalumu wa kufanikisha azma hiyo.

Imeelezwa kuwa jeshi la Israel limekuwa likitekeleza mashambulizi dhidi ya malengo yake kwa kasi kubwa, likifanikiwa mapema kuwaua baadhi ya viongozi wa juu wa Iran na kudhoofisha mifumo yake ya ulinzi.

Aidha, Israel inadaiwa kuharakisha operesheni zake kwa hofu kwamba Washington inaweza kufikia makubaliano na viongozi waliosalia wa Iran kabla malengo yake hayajatimia.

Ndani ya Iran, Israel ilishambulia makao makuu ya shirika la utangazaji la taifa hilo, Islamic Republic of Iran Broadcasting, yaliyoko Tehran.

 Aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa taifa la Iran, Ayatollah Ali Khamenei ambaye ameuawa kufuatia mashambulizi ya Israel na Marekani.

Wakati huohuo, wakazi wa Tehran wameonekana wakikimbia miji mikubwa huku barabara kuu zikijaa magari ya wanaoondoka kufuatia mashambulizi ya mabomu.

“Vita hivi vitaendelea kwa muda gani? Makazi ya kujikinga yako wapi? Serikali iko wapi?” amehoji Bijan (32), mfanyakazi wa benki, akizungumza kwa simu kutoka Tehran.

“Kila usiku mimi na mke wangu tunajificha chini ya jengo. Mji mzima uko kimya. Kila mahali kuna moshi na damu,” amesema.


Mpango wa Mossad

Ripoti mpya zimeibua madai mazito kuwa maofisa wa ujasusi wa Israel (Mossad) walidukua mtandao wa kamera za barabarani jijini Tehran kwa miaka kadhaa, wakifuatilia mienendo ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei, walinzi wake na maofisa wengine waandamizi kabla ya kuuawa kwake katika shambulio la anga mwishoni mwa wiki.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na Financial Times, Israel ilipata ufikiaji wa karibu kamera zote za jiji hilo, ambazo hutumiwa pia na Iran kufuatilia wapinzani wa utawala.

Picha na taarifa zilidaiwa kutumwa Tel Aviv, zikisaidia kujenga ramani ya kina ya ratiba, makazi na mienendo ya walinzi wa karibu wa Khamenei.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa pembe moja ya kamera karibu na makazi ya Khamenei katika Mtaa wa Pasteur ilikuwa muhimu, ikionyesha mahali walinzi walipokuwa wakiegesha magari yao binafsi, taarifa iliyodaiwa kusaidia kupanga operesheni ya mwisho.

Pia, gazeti hilo limeripoti kuwa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) ilikuwa na chanzo cha ndani kilichotoa taarifa muhimu kuhusu mahali alipokuwa Khamenei siku ya tukio.

Taarifa hizo ziliunganishwa na zana za akili bandia za Israel zilizochambua data kubwa ya mienendo ya viongozi wa Iran.

Mara baada ya kuthibitisha eneo la mkutano wa Khamenei, Israel na Marekani walidaiwa kuamua kuchukua hatua haraka kabla hajahamishiwa kwenye eneo la chini ya ardhi lenye kinga dhidi ya mabomu.