Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fahamu jinsi Kapteni Ibrahim Traoré alivyoingia madarakani

Rais wa Russia, Vladimir Putin alipokutana na Rais wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traoré wakati wa mkutano uliofanyika St. Petersburg, Julai 2023.

Muktasari:

  • Kapteni Ibrahim Traoré kwa sasa ndiye Rais wa Serikali ya Mpito ya Burkina Faso, umaarufu wake unazidi kuongezeka kila uchao kutokana na aina yake ya uongozi pamoja na uamuzi anaoufanya tangu achukue usukani wa kuongoza nchi hiyo

Dar es Salaam. Kapteni Ibrahim Traoré ni kiongozi kijana mwenye umri wa miaka 34 anayekabiliana na jukumu zito la kurejesha amani, usalama na maendeleo katika taifa ambalo limekumbwa na migogoro ya muda mrefu.

Hatima ya uongozi wake itategemea uwezo wake wa kushughulikia changamoto za kiusalama na kijamii huku akijenga imani ya raia na jumuiya ya kimataifa.

Hata hivyo, dhamira yake ya kuimarisha usalama na hali ya kiuchumi inaashiria mwanzo mpya kwa Burkina Faso.

Kapteni Ibrahim Traoré Kapteni wakati akitangaza mapinduzi ya Luteni Kanali Paul-Henri Damiba Septemba 30, 2022. Picha na Mtandao


Historia yake

Kapteni Ibrahim Traoré ambaye ni Rais wa Serikali ya Mpito ya Burkina Faso, ndiye kiongozi mdogo zaidi barani Afrika kwa sasa.

Mwanajeshi huyu amejipambanua kama mpinzani wa ‘mikakati isiyofanikiwa’ ya mtangulizi wake katika kupambana na makundi ya wanamgambo wa Islamic State na al-Qaeda.


Kuingia madarakani

Kapteni Traoré alimpindua Luteni Kanali Paul-Henri Damiba Septemba 30, 2022.

Hili lilikuwa jaribio la pili la mapinduzi ya kijeshi mwaka huo, likilenga kubadili mwelekeo wa mpito kuelekea utawala wa kiraia.

Traoré alijiunga na jeshi mwaka 2009 na kupanda ngazi haraka, akipata uzoefu wa uongozi katika operesheni mbalimbali nchini na kimataifa.

Alikuwa miongoni mwa wanajeshi waliomuunga mkono Damiba katika mapinduzi ya Januari 24 dhidi ya Rais Roch Marc Kabore.

Hata hivyo, baadaye aliikosoa Serikali ya mpito ya Damiba kwa kushindwa kuboresha hali ya usalama.


Maisha ya awali

Traoré alizaliwa mwaka 1988 huko Bondokuy katika Jimbo la Mouhoun.

Alipata elimu ya msingi huko kabla ya kuhamia Bobo-Dioulasso kwa masomo ya sekondari. Wanaomfahamu wanasema alikuwa kijana mwenye aibu, lakini mwenye akili nyingi.

Alijiunga na Chuo Kikuu cha Joseph Ki-Zerbo mjini Ouagadougou mwaka 2006, akihitimu kwa heshima.

Baadaye alijiunga na mafunzo ya kijeshi katika Chuo cha Georges Namoano kilichopo Po na alianza rasmi safari yake ya kijeshi mwaka 2009.

Alipandishwa cheo hadi Luteni mwaka 2014 na kapteni mwaka 2020, akihudumu katika vikosi mbalimbali ndani na nje ya nchi.


Ushujaa na mafanikio ya kijeshi

Kapteni Traoré alihudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa MINUSMA nchini Mali, alikoonesha ujasiri wakati wa shambulio la wanamgambo huko Timbuktu mwaka 2018.

Pia, aliongoza operesheni ya kijeshi mashariki mwa Burkina Faso mwaka 2019 iliyodumu kwa miezi saba na kuleta utulivu wa muda mfupi katika eneo hilo.


Maneno yake mwenyewe

Katika mahojiano na vyombo vya habari, Traoré alifafanua sababu za mapinduzi, akisema:

“Makubaliano yetu ya pamoja yalisalitiwa na kiongozi wetu. Kuzorota kwa hali ya usalama, jambo lililotufanya kuchukua hatua kwa masilahi ya kisiasa.

“Sikuamua kuchukua madaraka; nilichaguliwa na wanajeshi wenzangu baada ya kushindwa kupata suluhu kupitia mazungumzo.

“Katika miezi mitatu ijayo, lazima tufanye kazi kubwa kurekebisha mambo yaliyoshindikana kwa miezi minane iliyopita.”


Vipaumbele vyake

Baada ya kuingia madarakani, Traoré aliahidi kupambana na makundi ya kigaidi ili kurejesha usalama.

Pia, aliahidi kuboresha hali ya kiuchumi, kuimarisha miundombinu na kupambana na ufisadi.

Kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na mataifa ya Afrika na washirika wengine wa kimataifa.


Changamoto anazokabiliana nazo

Traoré anakabiliwa na changamoto kubwa, zikiwemo za vita dhidi ya makundi ya kigaidi, hasa kaskazini na mashariki mwa Burkina Faso.

 Changamoto nyingine ni kukosekana kwa imani ya raia kutokana na kuondolewa kwa viongozi wawili wa kijeshi katika kipindi kifupi.

Pia, shinikizo la kurejesha utawala wa kiraia huku akipambana na matatizo ya kisiasa na kiusalama.