Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taifa Gas yalinda watumiaji bei ya gesi ya kupikia ikipaa

Meneja Mkuu wa Taifa Gas, Devis Deogratius

Muktasari:

  • Uamuzi huo unalenga kulinda watumiaji dhidi ya athari za mabadiliko ya bei duniani, huku ikiendelea kuhakikisha upatikanaji wa nishati safi kwa gharama nafuu.

Dar es Salaam. Kampuni ya Taifa Gas imetangaza kuwa haitapandisha bei ya gesi ya majumbani (LPG), licha ya kupanda kwa bei ya nishati hiyo katika soko la kimataifa kwa takribani asilimia 43 katika wiki za hivi karibuni.

Uamuzi huo umetajwa kuwa sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo kulinda watumiaji dhidi ya athari za mabadiliko ya bei duniani, huku ikiendelea kuhakikisha upatikanaji wa nishati safi kwa gharama nafuu.

Taarifa hiyo, imetolewa leo, Ijumaa Aprili 3, 2026 na Meneja Mkuu wa Taifa Gas, Devis Deogratius, alipozungumza na waandishi wa habari.

Amesema ongezeko la bei katika soko la kimataifa limeongeza gharama za ununuzi na usambazaji wa gesi, lakini kampuni imechukua hatua ya kubeba mzigo huo ili kuwasaidia wateja wake.

“Katika mazingira haya ya sasa, tunayo dhamira ya dhati ya kuwasaidia wateja wetu kwa kubeba athari za ongezeko la gharama ya nishati ya kupikia kwa kutokuongeza bei huku tukihakikisha upatikanaji endelevu wa gesi safi na ya kuaminika,” amesema Deogratius.

Kwa upande wake, Meneja wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Oscar Shelukindo, amesisitiza uamuzi huo unaakisi dhamira ya Taifa Gas ya kuchangia ustawi wa jamii na uchumi wa nchi kwa ujumla.

“Tunatambua umuhimu wa gesi ya kupikia katika maisha ya kila siku ya Watanzania, hususan kwa kaya na wafanyabiashara wadogo. Kwa kuendelea kushikilia bei, tunalenga kupunguza mzigo wa gharama kwa wananchi na kuchochea shughuli za kiuchumi,” amesema.

Ameongeza kuwa licha ya changamoto za soko la kimataifa, kampuni hiyo imewekeza katika miundombinu ya usambazaji ili kuhakikisha huduma inawafikia wananchi kwa uhakika mijini na vijijini.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, Taifa Gas inaendesha mtandao wa maghala 25 nchini kote, jambo linaloiwezesha kusambaza gesi kwa ufanisi katika maeneo mbalimbali yenye mahitaji tofauti.

Mbali na kulenga utulivu wa bei, Taifa Gas pia imeendelea kuunga mkono juhudi za kitaifa na kimataifa za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. Hatua hiyo inalenga kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, kulinda mazingira, na kuboresha afya za wananchi.

Shelukindo, amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kufuatilia mwenendo wa soko la kimataifa na kushirikiana na wadau wa sekta ya nishati ili kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake.

“Dhamira yetu ni ya muda mrefu kuhakikisha Watanzania wanapata nishati safi, nafuu na ya kuaminika, huku tukizingatia uwajibikaji katika uendeshaji wetu,” amesisitiza.

Taifa Gas ni miongoni mwa kampuni zinazoongoza nchini katika usambazaji wa gesi ya majumbani, ikiwa na kituo kikubwa zaidi cha kuhifadhi LPG pamoja na mtandao mpana wa usambazaji unaoifikia sehemu kubwa ya nchi.