Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mradi wa PTE wawaokoa watoto walio hatarini kuacha shule

Balozi wa Italia nchini Tanzania, Giuseppe Coppola akizungumza katika hafla ya kufunga mradi wa Pamoja Tudumishe Elimu (PTE) uliodumu kwa miaka mitatu nchini Tanzania.

Muktasari:

  • Washirika wa kimataifa waungana kuinua ubora wa elimu, kuboresha mazingira ya watoto kwenda shuleni.

Dar es Salaam. Watoto waliokuwa katika hatari ya kuacha shule kutokana na umaskini, ajira za utotoni, ukatili, ulemavu na mazingira duni ya kujifunzia wamepata fursa mpya ya kuendelea na masomo baada ya utekelezaji wa mradi wa Pamoja Tudumishe Elimu (PTE), uliodumu kwa miaka mitatu nchini Tanzania.

Badala ya kujikita tu katika kuwapeleka watoto darasani, mradi huo ulitumia mbinu shirikishi iliyohusisha shule, wazazi, jamii na taasisi za serikali ili kushughulikia sababu zinazowafanya watoto washindwe kuendelea na masomo.

Mradi huo uliotekelezwa na shirika la WeWorld kwa ushirikiano na mpango wa Educate A Child wa Education Above All (EAA) Foundation, ukifadhiliwa na Qatar Fund for Development, ulitekelezwa katika manispaa za Temeke na Kinondoni jijini Dar es Salaam na katika kaunti za Migori na Narok nchini Kenya.

Watoto wakionesha igizo katika hafla ya kufungwa kwa mradi wa wa mradi wa Pamoja Tudumishe Elimu (PTE) uliodumu kwa miaka mitatu nchini Tanzania.

Viongozi wa WeWorld wakizungumza wakati wa kufunga rasmi mradi huo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wamesema mafanikio makubwa yaliyopatikana ni kuongezeka kwa ushiriki wa watoto katika elimu, kuboreka kwa mazingira ya kujifunzia na kuongezeka kwa uwezo wa shule pamoja na jamii kuwabaini na kuwasaidia watoto walio katika hatari ya kuacha shule.

Kwa mujibu wa shirika hilo, changamoto zilizokuwa zikiwakwamisha watoto kuendelea na masomo zilikuwa si za kielimu pekee, bali pia za kijamii na kiuchumi. Hivyo, suluhisho lilihitaji ushirikiano wa sekta mbalimbali badala ya shule peke yake.

Ofisa kutoka Ofisi ya Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu, Dk Richard Chiligati alisema mimba za utotoni, changamoto za malezi na makuzi maeneo ya nyumbani na ushiriki wa jamii katika kufuatilia ufundishwaji wa wanafunzi mambo haya yanachangia kuacha wanafunzi kuacha shule.

“Miradi kama hii inatusaidia katika kuboresha elimu hasa kwenye utatuzi wa changamoto hizi. Serikali kwa sasa imehamasisha jamii kutoa chakula shuleni ambapo suala la kuacha limepungua. Walimu pekee hawawezi tumekuwa tukiwaita wazazi kuelimisha juu ya ulinzi wa watoto,” alisema.

Watoto wakionesha igizo katika hafla ya kufungwa kwa mradi wa wa mradi wa Pamoja Tudumishe Elimu (PTE) uliodumu kwa miaka mitatu nchini Tanzania.

Katika utekelezaji wake, mradi uliongozwa na mfumo wa CARES Framework for Child-Centred Education, unaojengwa katika nguzo tano muhimu. Nguzo hizo ni ushiriki wa jamii katika kukuza elimu ya watoto, kuongeza upatikanaji wa elimu jumuishi, kulinda haki za watoto, kutoa nafasi kwa watoto kueleza maoni yao pamoja na kuhakikisha usalama wao ndani na nje ya mazingira ya shule.

Kupitia mfumo huo, wazazi na viongozi wa jamii walihamasishwa kushiriki katika malezi na elimu ya watoto, walimu waliinuliwa uwezo wa kuwahudumia wanafunzi wenye mahitaji mbalimbali, huku shule zikisaidiwa kujenga mazingira rafiki yanayowezesha watoto wote kujifunza bila ubaguzi.

Balozi wa Italia nchini Tanzania, Giuseppe Coppola, alisema mradi huo umeonyesha namna ushirikiano wa kimataifa unavyoweza kuleta matokeo makubwa katika sekta ya elimu.