Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matumizi ya fedha hizi Tanzania mwisho kesho

Muktasari:

  • Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema mwisho wa kutumia matoleo ya fedha ilizoziainisha (pichani) ni kesho Jumamosi Aprili 5, 2025 huku ikitoa angalizo kuwa baada ya hapo hazitatambulika tena.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema mwisho wa kutumia matoleo ya fedha ilizoziainisha (pichani) ni kesho Jumamosi Aprili 5, 2025 huku ikitoa angalizo kuwa baada ya hapo hazitatambulika tena.

“Hatua ya ubadilishwaji wa noti za zamani ilianza Januari 6, 2025 itamalizika Aprili 5, 2025 ambapo matumizi ya noti hizo yatafikia ukomo wa kuwa fedha halali za Tanzania.

“Baada ya tarehe hiyo, mtu yeyote au taasisi yoyote inayomiliki fedha hizo haitaruhusiwa kuzitumia katika kufanya malipo popote nchini; na benki zote hazitaruhusiwa kulipa wala kupokea amana au maombi ya kubadilisha noti zilizoondolewa kwenye mzunguko,”imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa katika mitandao ya kijamii ya BoT jana Aprili 3, 2025.

Wengi wamekuwa wakijiuliza ni noti zipi ambazo zimetangazwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuwa zitaondolewa kwenye mzunguko wa matumizi kati ya  Januari na Aprili mwakani.

Oktoba 24, 2024 tangazo la kwanza la Bot ilitangaza kuziondoa noti za Sh20, Sh200, Sh500, Sh1,000, Sh2,000, Sh5,000 na Sh10,000 zilizotolewa kuanzia mwaka 1985 hadi 2003, pamoja na noti ya Sh500 iliyotolewa mwaka 2010.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Gavana wa benki hiyo, Emmanuel Tutuba, ilihusisha Tangazo la Serikali Na. 857 na 858 lililochapishwa Oktoba 11, 2024 ambalo limetoa wito wa kuwasilisha, kuweka au kubadilisha, na kusitisha matumizi ya noti za zamani.


Taarifa hiyo ilieleza kuwa kazi hiyo itaendelea kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari 6, 2025 hadi Aprili 5, 2025, noti hizo zitakapositishwa kuwa sarafu halali.

“Zoezi la ubadilishwaji linatarajiwa kuanza  Januari 6, 2025 hadi Aprili 5, 2025 kupitia Ofisi zote za Benki Kuu na benki zote za biashara kwa kupatiwa malipo yenye thamani sawasawa na kiasi kitakachowasilishwa,” ilisema taarifa hiyo.

Akifafanua zaidi kuhusu hatua hiyo Kaimu Mkurugenzi wa usimamizi wa Sarafu wa BoT, Ilulu Ilulu alisema zoezi hilo si geni kwa mamlaka hiyo yenye jukumu la pekee la kuchapisha noti na kuzisambaza nchini Tanzania kwa sheria ya mwaka 2006 sura ya 197.

“Kupitia kifungu cha 28 (2) na (3) ya Sheria hiyo, Benki Kuu imepewa mamlaka ya kusitisha uhalali ya fedha itakazozianisha kadri itakavyoona inafaa kwa kuchapisha tangazo katika Gazeti la Serikali,” alisema.

Ilulu alisema inapotokea kusitisha uhalali wa noti fulani wananchi hupewa muda maalumu wa kuzibadilisha kabla ya kusitisha uhalali huo na hupewa fursa ya kubadilisha noti husika kwa kupewa kiwango kile kile.