Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ijue mitego hii ya ulaghai katika huduma za kidijitali

Urahisi wa kufanya miamala kwa simu au kompyuta umebadilisha namna tunavyohifadhi na kutuma fedha, lakini umewapa pia wahalifu fursa ya kubuni mbinu mpya za kuwalenga watumiaji wasiokuwa waangalifu. Ili kubaki salama, tunahitaji kuelewa hila hizi na kuchukua tahadhari kabla ya hasara.

Mbinu ya kwanza ni ile ya ujumbe bandia unaodai tatizo la akaunti. Matapeli wanaweza kutumia namna hiyo hujitambulisha kama mtoa huduma mfano benki au kampuni ya simu, kisha hutuma barua pepe au SMS zenye maneno yanayokuweza kukupa wasiwasi mfano “akaunti yako imefungwa” au “malipo yamekwama”.

Kuondoa changamoto hiyo unaweza kupokea ujumbe kufuata kiungo fulani (link), au tuma neno lako la siri tukusaidie, na mengineyo.

Mbinu za namna hiyo inaweza kuwa ni mtego kunasa neno la siri au PIN yako. Kumbuka, taasisi halali hazitumi ombi la PIN kupitia viungo visivyo rasmi; ukipokea ujumbe wa aina hii, usihadaike, na kwa uhakika wasiliana na mtoa huduma kwa nambari inayojulikana kuepuka kunasa katika mtego.

Njia nyingine hutumia programu hasidi katika kompyuta au kifaa cha kielektroniki. Kwa mfano kupitia faili au programu unazopakua kutoka kwenye vyanzo visivyoaminika kuingia katika simu au kompyuta yako na kuweza kusoma taarifa zako muhimu mfano kuiga skrini zako wakati unafanya miamala na kuzipeleka kwa mdukuzi.

Kinga bora ni kupakua programu kutoka katika vyanzo vilivyohakikiwa kwa mfano tovuti rasmi, na kuepuka kufuata kila kiungo link unayotumiwa au kuiona mtandaoni.

Vilevile walaghai hutumia ushawishi wa kisaikolojia. Baadhi yao kwa njia ya simu kupiga au kwa kutembelea waathiriwa wakijifanya maofisa kutoka taasisi fulani, wanaweza kutaja baadhi ya taarifa zako binafsi kama jina, unapokaa ili uweze kuwaamini na kukushawishi utoe taarifa fulani nyeti ambayo inaweza kukusaidia.

Ni vyema katika wakati kama huo kujiridhisha, kwa kuwasiliana na watoa huduma, mfano kupiga namba rasmi ya taasisi husika kabla hujatoa maelezo. Lakini jambo la msingi zaidi kujua taasisi za kifedha si kawaida kuagiza watu nyumba kwa nyumba kukusanya PIN wala nambari ya kadi, au kukupigia kwa namba isiyo rasmi kukudai maelezo, ukikutana na mazingira hayo tia shaka.

Mbinu nyingine ni kupitia Wi‑Fi za umma. Intaneti inayopatikana dukani au stendi mara nyingi haina usimbaji fiche unaohitajika kulinda taarifa zako. Mdukuzi aliye kwenye mtandao huo anaweza kunasa mawasiliano yako. Jambo la muhimu ni kuepuka kujiunga na kila WIFI unayokutana nayo kwenye kifaa chako.

Wapo watumiaji wanaojikuta wakitoa nambari zao za siri kwa mawakala wa huduma za fedha kwa simu, pengine kwa sababu hawajui jinsi ya kutoa pesa wenyewe. Katika mazingira yetu si jambo la kushangaza kuona mtu anampa wakala simu na PIN yake ili amsaidie kuvuta fedha.

Hata hivyo, PIN ni taarifa ya siri kabisa; mtu mwingine akiijua, usalama wa akaunti yako unakuwa hatarini. Ukimpa mtu nambari hiyo, na ikitokea ana nia mbaya, anaweza kutumia fursa hiyo baadaye kujihamishia fedha zako kama atakavyo. Jifunze hatua za kufanya muamala au tafuta msaada bila kufichua siri zako.

Kujilinda kunahitaji nidhamu ya kila siku. Tumia neno siri imara na usilirudie kwenye akaunti nyingine, kagua taarifa zako mara kwa mara ili kugundua kama kuna muamala usio wa kawaida mapema, na endelea kuhuisha programu pamoja na mfumo wa uendeshaji wa kifaa chako ili kuziba mianya ya kiusalama.

Ukiwa na maarifa sahihi na tahadhari, unaweza kufurahia urahisi wa huduma za fedha kidijitali bila kuogopa mitego ya wahalifu.