Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bei ya nyama Dodoma, Dar yapanda

Muuza nyama akiwa ofisi kwake

Muktasari:

Yaelezwa sababu ni kupanda kwa ng’ombe na ukame wanakotoka

Dodoma. Wafanyabiashara wa nyama ya ng’ombe katika Manispaa ya Dodoma, wametangaza kupandisha bei ya nyama ya ng’ombe kutoka Sh6,000 hadi Sh7,000 kwa kilo moja.

Bei hiyo mpya ilibandikwa katika bucha za nyama mjini hapa kuanzia jana.

Wakati Dodoma bei mpya ikibandikwa, jijini Dar es Salaam nyama imepanda kimyakimya kutoka Sh6,000 kwa kilo hadi Sh 8,000 na maeneo mengine kama Mbagala kilo moja inauzwa hadi Sh10,000.

Akizungumzia kupanda kwa bei ya nyama mjini Dodoma jana, mmoja wa wauzaji wa nyama, Ally Kalumbo alisema kupanda kwa bei ya kitoweo hicho inatokana na uhaba wa ng’ombe.

“Kwa sasa tumeweka matangazo ili kuwataarifu wateja wetu juu ya

kupandishwa kwa bei, ili wanapokuja kununua nyama wawe wana taarifa kamili,” alisema.

Alipoulizwa kuhusiana na kupanda kwa bei hiyo, Mwenyekiti wa Wauza Nyama ya Ng’ombe mjini Dodoma, Thomas Kuhura alisema hatua hiyo inatokana na kupanda kwa bei ya ng’ombe.

“Pia kutokana na ukame unaokabili maeneo mbalimbali ya nchi ng’ombe wana hali mbaya, hawana uzito mkubwa,” alisema.

Naye Meneja Uzalishaji wa Machinjio ya Kisasa mjini humo, Khamis Kissoi alisema kuna tatizo la upatikanaji wa ng’ombe na kwa sasa wamekuwa wakipokea chini ya ng’ombe 180 kwa siku.

Alisema siku za Jumapili ng’ombe wanaochinjwa wameshuka hadi 150 na kwamba, uchinjaji katika machinjio hayo umeshuka kwa asilimia 15, suala ambalo limechangia kupanda kwa bei.