Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UDSM yapiga mkwara, BDL kupingwa viwanja viwili

Muktasari:

  • Katika fainali hiyo JKT iliifumua UDSM katika michezo 3-1 ambapo katika mchezo wa kwanza JKT ilishinda pointi 67-62, ule pili UDSM ikashinda 66-55 ilhali ule wa tatu na wa nne JKT ikishinda kwa pointi 68-58 na 75-50 mtawalia.

JOTO la ufunguzi wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) kati ya UDSM Outsiders na JKT linazidi kupanda kutokana na kumbukumbu ya ushindani uliotokea katika fainali ya mashindano hayo mwaka jana.

Katika fainali hiyo JKT iliifumua UDSM katika michezo 3-1 ambapo katika mchezo wa kwanza JKT ilishinda pointi 67-62, ule pili UDSM ikashinda 66-55 ilhali ule wa tatu na wa nne JKT ikishinda kwa pointi 68-58 na 75-50 mtawalia.

Kocha wa UDSM Outsiders, Mohamed Mgweno ameitahadharidha JKT isiuchukulie mchezo huo kuwa mwepesi kufuatia nyota wake Evance Davies, Mwalimu Heri na Tyrone Edrward kutimkia Stein Warriors akidai wako fiti na watatoa upinzani mkali.   

“Timu yangu imejipanga vizuri kuikabili JKT katika mchezo wa ufunguzi siku ya Jumamosi (Mei 10),”  alisema Mgweno, huku akidai mchezo huo utakuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa kutokana na uzoefu wa wachezaji wa timu hizo mbili. 

Akizungumzia wachezaji waliowasajili, alisema wameongeza wachache waliocheza Ligi ya Daraja la Kwanza msimu uliopita ingawa hakutaja majina.

Kwa upande wa JKT ambao ndiyo bingwa mtetezi wa ligi hiyo, inajivunia kuwa na mastaa Jordan Manang, Baraka Sabibi, Omary Sadiki, Alfan Mustafa na Adam Lutungo.


DB LIONESS VS VIJANA QUEENS

Mchezo mwingine wa ushindani utakuwa ni ule wa Ligi ya Kikapu ya Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam (WBDL), kati ya DB Lioness na Vijana Queens.  

DB Lioness ambayo ndiyo bingwa mtetezi wa ligi hiyo, iliivua ubingwa Vijana Queens kwa kuifunga michezo 3-2. Mchezo huo utatangulia kabla ya mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo kati ya JKT na UDSM Outsiders unaofanyika Jumamosi katika Uwanja wa Donbosco, Upanga. Upinzani wa timu hizo ni kama ulivyo wa kaka zao, Savio na Vijana ‘City Bulls’. 

Timu ya Lioness inamtegemea Taudencia Katumbi ambaye ni raia wa Kenya, huku Vijana Queens ikimtegemea Noela Renatus.

Taudencia katika ligi hiyo mwaka jana aliichangia timu hiyo kutwaa ubingwa wa WBDL baada ya kushika nafasi ya pili kwa ufungaji wa pointi 501.

Nyota huyo pia alishika nafasi ya pili kwa kudaka mipira ya ‘rebound’ mara 341 na upande wa kuzuia ‘block’ alishika nafasi ya 10 kwa kuzuia mara 25. Kwa upande wa timu ya Vijana Queens ni Noela Renatus aliyeshika nafasi ya tatu na kwa kutoa asisti mara 103 ilhali upande wa kupokonya mipira (steals) alishika nafasi ya tano baada ya kupokonya mara 32.


VIWANJA VIWILI BDL

Akizungumzia mashindano hayo, Kamishna wa Ufundi na Mashindano wa BDL, Haleluya Kavalambi alisema viwanja viwili vinatarajiwa kutumika kuchezewa mashindano hayo.

“Tumeamua hivyo kwa lengo la kutaka ligi hiyo imalizike kwa wakati,”  alisema Kavalambi akitaja viwanja hivyo kuwa ni ule wa ndani wa Donbosco Upanga pamoja na wa nje. Kwa mujibu wa Kavalambi michezo itakayochezwa siku ya ufunguzi, Jumamosi itakuwa minne kati ya Twalipo Queens na City Queens, ilhali Kurasini Heat itakipiga na Mgulani JKT, DB Lioness itaikaribisha Vijana Queens na mchezo wa ufunguzi utakuwa kati ya JKT na UDSM Outsiders.

Alisema ligi hiyo itaendelea Jumapili kwa michezo saba na kwamba wiki ijayo itaendelea katika siku za Alhamisi, Ijumaa, Jumamosi na Jumapili.