Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

PUMZI YA MOTO: Simba na Mashujaa hazijawahi kutuangusha

PUMZI Pict

Muktasari:

  • Achana na kilele za siku mbili hizi kwamba Mashujaa inadhaminiwa na kampuni yenye maslahi na wapinzani wa Simba, ndio maana wakaikazia sana Simba. 

HEBU tumuweke pembeni kidogo Kefa Kayombo na msaidizi wake namba moja, Neema Wilson Mwambashi walioamua mechi ya Simba na Mashujaa, Mei 2, 2025. Tuziangalie timu hizo zinapokutana na ushindani unaokuwepo. Mechi ya Mashujaa na Simba haijawahi kuwa ya polepole hata kidogo.

Achana na kilele za siku mbili hizi kwamba Mashujaa inadhaminiwa na kampuni yenye maslahi na wapinzani wa Simba, ndio maana wakaikazia sana Simba. Rudi nyuma hata kabla ya udhamini huo. Hata kabla Mashujaa haijapata daraja kucheza Ligi Kuu Bara. Rudi nyuma hadi Desemba 26, 2018 kwenye Uwanja wa Mkapa.

Mashujaa ikiwa Ligi Daraja la Kwanza iliichapa Simba 3-2 na kuitoa katika hatua ya 64 bora ya Kombe la Shirikisho (FA). Hilo lilikuwa ni moja ya matukio yanayokumbushia stori maarufu ya Daudi kumpiga Goliati. Na hata Mashujaa ilipokuja kupanda daraja baadaye hali iliendelea kuwa vivyo hivyo. Mechi dhidi ya Simba huwa mechi kwelikweli, hata kama itapoteza.

Msimu uliopita Mashujaa walipoteza mechi zote mbili kwa Simba, lakini haikuwa kinyonge. Mpira ulipigwa haswa na washindi kuona kwamba mshahara wa siku hiyo wameufanyia kazi hasa. Machi 15, 2024 matokeo yalikuwa Simba 2-0 Mashujaa ilhali Februari 3, 2024 ilikuwa Mashujaa 0 - 1 Simba.

PUM 01

Na zilipokutana kwenye Kombe la Shirikisho (FA) Mashujaa ikalipa kisasi na kuitoa Simba katika mechi ile ya Aprili 9, 2024 ambayo matokeo yalikuwa Mashujaa 1-1 Simba (penalti: 6-5).

Kwa kifupi ni kwamba ziligawana furaha, Simba ilifurahia ushindi katika Ligi na Mashujaa ilifurahia ushindi kwenye Kombe la Shirikisho. Msimu huu pia Simba imeshinda mechi zote za ligi yaani ile ya Mei 2, 2025 kwa mabao 2-1 na awali Novemba Mosi, 2024 bao 0-1.

Mashujaa haina sehemu ya kutafuta furaha kama msimu uliopita kwa sababu hakuna mashindano mengine yaliyobaki yatakayozikutanisha. Lakini licha ya Simba kushinda mechi hizo bado walilala na viatu. Mechi zote mbili ziliamuliwa dakika moja ya mwisho - baada ya vita kali kiwanjani.

PUM 02

Simba ilipewa mechi za uhakika hasa, zile mechi ambazo hukutana nazo dhidi ya wakubwa wenzake. Ni bahati mbaya tu kwamba mpira wetu umejengewa misingi ya kutoheshimu wengine zaidi ya Simba na Yanga. Inapotokea wababe hao wawili wanakutana na ushindani mkali unaojirudia kutoka timu fulani, basi hutafutwa tafsiri nyingine isiyo ya kimpira kuielezea hali hiyo.

Sababu huwa mbili tu; unatumika na mpinzani au unakamia. Kwa mfano kwa Mashujaa na Simba ndio utasikia unajadiliwa udhamini - kwamba Mashujaa inajitoa zaidi ya kawaida ili kumnufaisha mdhamini ambaye pia anahusika na wapinzani wao.

Kwa hiyo Mashujaa inatumika na wapinzani wa Simba, ilhali ukweli ni kwamba wanajeshi hao walianza 'ukorofi' kwa Simba, hata kabla ya huu udhamini.

PUM 03

Na hii sio Tanzania tu, duniani kote iko hivyo. Utakuta timu fulani kubwa na imetawala soka la nchi, lakini kanatokea katimu kamoja kadogo tu kanaisumbua sana. Hata kama hao wakubwa watashinda, lakini watalala na viatu. Msimu wa 2022/23, Brighton ilijipatia sifa hiyo katika Ligi Kuu England. Ilinyanyasa sana wakubwa huku ikiteseka kwa 'watoto wenzao'.

Katika msimu huo Agosti 7, 2022 matokeo yalikuwa Manchester United 1–2 Brighton; Oktoba Mosi, 2022 Liverpool 3–3 Brighton; Oktoba 28, 2022 Brighton 4–1 Chelsea; Januari 14, 2023 Brighton 3–0 Liverpool; Aprili 15, 2023 Chelsea 1–2 Brighton; Mei 4, 2023 Brighton 1–0 Manchester United; Mei 14, 2023 Arsenal 0–3 Brighton na Mei 24. 2023 Brighton 1–1 Manchester City.

Wakati ikipata matokeo hayo dhidi ya wakubwa, hebu ona baadhi ya matokeo dhidi ya wadogo wenzao. Aprili 26, 2023 Nottingham Forest 3–1 Brighton; Mei 8, 2023 Brighton 1–5 Everton na Mei 18, 2023 Newcastle United 4–1 Brighton. Yaani  Mei 14, 2023 ilitoka kushinda 3-0 ugenini kwa Arsenal, halafu ikaenda kufungwa mabao 4-1 kwa Newcastle.

PUM 04

Huo ndio mpira  na ndicho inachotuletea Mashujaa. Yawezekana aina ya uchezaji inaipa tabu sana Simba kiasi cha kutumia nguvu nyingi kushinda. Na katika saikolojia ya kawaida ni rahisi Mashujaa kujihamasisha dhidi ya Simba kupitia matokeo ya zamani. "Kama tuliwafunga Simba tukiwa daraja la kwanza, kwanini tuwashindwe sasa tukiwa Ligi Kuu?"

Kauli hiyo ikiingia kwenye mioyo ya wachezaji na kuamini inawezekana lazima hali itakuwa tofauti. Ni kama ule msemo wa maisha ya porini. Kwamba wakati wanyama wengine wanamuangalia tembo kama mnyama mkubwa, Simba inamuangalia tembo kama chakula. Yaani akimuona tu anakuwa ameiona 'lunch' sio mnyama mkubwa kama wanavyomuona wengine. Na usikute hiyo ndio hali ya Mashujaa. Ikiiona Simba inakuwa imeuiona ushindi, sio wanafainali wa Afrika. Inaingia uwanjani kuufuata ushindi wake kama ilioupata 2018.

PUM 05

Sasa hali hiyo ndio wengine huweza kuitafsiri kama kutumika au kukamia. Lakini kwa kweli Mashujaa na Simba hutupa mechi bora sana mara zote. Bahati mbaya sana kocha wa zamani wa Yanga, Sead Ramovic aliondoka kabla hajakutana na hali kama hii. Ndiyo maana akasema ligi ya Tanzania haina kiwango kizuri cha ushindani. Lakini kama angeendelea kubaki angalau msimu mzima angebadilisha kauli.