Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

New King yatanguliza mguu mmoja ZPL 

KING Pict

Muktasari:

  • Hatua ya mtoano wa Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Unguja imeanza jana Jumatatu kwenye Uwanja wa Mao A, kwa kuzikutanisha  Sebleni na New King.

SHIRIKISHO la Soka Zanzibar(ZFF) limeanza kusaka timu nne zitakazopanda daraja  kucheza Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) msimu ujao, ili kichukua nafasi ya zile zitakazoshuka katika Ligi hiyo ya juu ngazi ya klabu visiwani humu.

Hatua ya mtoano wa Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Unguja imeanza jana Jumatatu kwenye Uwanja wa Mao A, kwa kuzikutanisha  Sebleni na New King.

Katika mtanange huo wa raundi ya kwanza New King iliichapa Sebleni kwa mabao 3-2. 

Ushindi huo umeiweka New King ilitolewa robo fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) wikiendi iliyopita katika nafasi nzuri ya kupanda Ligi Kuu kuchukua nafasi ya timu nne zitakazoshuka, zikiwamo tatu za New City, Inter Zanzibar na Tekeleza zilizotangulia mapema.

Inter Zanzibar na Tekeleza zilipanda daraja msimu huu sambamba na vinara wa Ligi Kuu kwa sasa, Mwembe Makumbi na Junguni United, lakini zenyewe zimeshindwa kushikilia bomba.

Kipute cha hatua hiyo ya mtoano ya kusaka timu za kupanda daraja kitaendelea leo Jumanne kwa Polisi na Kundemba kuonyeshana kazi kwenye Uwanja wa Mao A kuanzia saa 10 jioni.

Polisi na Kundemba zilishuka daraja msimu uliopita katika Ligi Kuu Zanzibar sambamba na Hard Rock na Maendeleo.