Siku ya Mtoto wa Afrika: Elimu jumuishi kwa watoto na kujenga kizazi hodari chenye maarifa, maadili na stadi za kazi

Mwalimu wa malezi Shule ya Msingi Mang'onyi,  Akwelina S kimaro akiwaongoza wanafunzi vinara wa elimu rika kuelezea uelewa wao juu ya ukatili wa kijinsia na kutoa elimu kwa wanafunzi wenzao wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida na kuratibiwa na Mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kaskazini Mashariki kupitia ofisi ya Singida.


Ikiwa ni mwaka wa 33 tangu kuanza kuadhimishwa kwa Siku ya Mtoto wa Afrika mnamo mwaka 1991, Siku hii muhimu imeadhimishwa mwaka huu bara la Afrika likiwa linakadiriwa kuwa na watoto (umri 0-17) zaidi ya milioni 650. Kwa mujibu wa shirika la Kimataifa la kuhudumia watoto Ulimwenguni UNICEF, ifikapo mwaka 2055, Afrika inakadiriwa kuwa na idadi ya watoto billioni moja.

Kaulimbiu ya maadhimisho haya mwaka huu ni "Elimu Jumuishi kwa Watoto izingatie: Maarifa, Maadili na Stadi za Kazi". Kauli mbiu hii inaakisi umuhimu wa ‘Elimu, Maadili na Stadi za Kazi’ bora katika ulimwengu huu wa sasa unaohitaji watu wenye maarifa mbalimbali, wenye maadili katika utendaji wa kazi na ujuzi kwenye nyanja mbalimbali.

Kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR), kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID); Mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kaskazini Mashariki unaotekelezwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - Makao Makuu (KKKT), unatekeleza afua mbalimbali zinazochangia juhudi za Serikali katika kuhakikisha Afya, Elimu, Ulinzi na Kukuza Uchumi wa Kaya kwa Ustawi wa mtoto na familia yake.

Mradi huu unatambua umuhimu wa elimu jumuishi na huduma mbalimbali katika kutoa elimu, kuzingatia maadili na kujenga ujuzi wa stadi mbalimbali za maisha. Mradi huu unashirikiana na Serikali na wadau wengine kufikia Watoto walio katika mazingira hatarishi na walezi wao katika mikoa ya utekelezaji wa mradi. Mikoa hii ni Arusha, Dodoma, Geita, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Mwanza, Singida na Tanga.

Programu ya kuzuia maambukizi ya VVU na vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto (DREAMS)

Mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kaskazini Mashariki unatekeleza programu ya DREAMS (Determined, Resilient, Empowered, AIDS-free, Mentored, and Safe) Katika Mkoa wa Mwan¬za. Programu hii inaweza kutafsiriwa nakuleta maana ya mwenye Nia, Ustahimilivu, Kuwe z e s hwa, Kujitambua, kujil¬inda dhidi ya VVU/UKIMWI, na Salama. Hii ni programu inayotumia Ushahidi wa kisay¬ansi katika kuweka mikakati ya kuzuia maambukizi ya Virusi Vya UKIM¬WI (VVU) kwa kutatua changa¬moto zinazofanya vijana wa kike na kiume kuwa hata¬rini kupata maambukizi ya VVU. Afua hii inalenga kuwafikia watoto wa shule wenye umri wa miaka 10-17 ili kutoa elimu ya kujikinga dhidi ya magonjwa hatarishi kama VVU na kujikinga na unyanyasaji wa kijinsia na tabiahatari¬shi katika Mkoa wa Mwanza.

Afua ya kwanza ya utekelezaji wa mipango ya kuzuia maambukizi ya VVU na vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto (Core DREAMS)

Afua ya kwanza ya programu ya ‘DREAMS’ imejikita katika kuwezesha wasichana balehe katika shule za Msingi wenye miaka (10-14) kupata elimu ya Afya ya Uzazi, elimu ya fedha, kupata vifaa vya shule na taulo za kike za hedhi zinazotumika zaidi ya mara moja.

Lengo la programu hii ni kuwezesha wasichana kuweza kuendelea kue-ndelea na masomo yao na kuwaepusha na tabia zinazoweza kupelekea kupata maambukizi ya VVU au ukatili wa aina yoyote. Hadi kufikia Juni 2024, jumla ya wasichana 11,482 walikuwa wamefikiwa na programu hii katika Halmashauri ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza.


Elimu ya Fedha

Lengo namba 4 katika Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa linaku-sudia kuhakikisha elimu bora yenye usawa na jumuishi. Ili kuhakikisha vijana wanapata maarifa na ujuzi utakao wawezesha kushiriki kika¬milifu na kusaidia kupunguza vikwazo mbalimbali vya kiuchumi. Kupitia mtaala wa elimu ya fedha, DREAMS inawezesha wanafunzi katika shule za Msingi na Sekondari kupata elimu ya fedha na kuwawezesha kupata maarifa ya kupanga bajeti na kuweka akiba kwa mahitaji ya baadae.


Vifaa vya Usafi wakati wa Hedhi

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto Ulimwenguni (UNICEF), mamilioni ya wasichana balehe duniani kote wanakosa haki ya kufurahia hedhi salama. Kupitia ‘DREAMS’ wasichana wanapata taulo za kike zinazoweza kutumika zaidi ya mara moja na shule zinahamasishwa kuwa na vyumba maalumu vya kubadilishia. Lengo ni kusaidia wasichana kudumisha usafi wa hedhi na hivyo kuongeza mahudhurio yao darasani. Hii itasaidia kuhakikisha wasichana wanaendelea kupata elimu na kufura¬hia masomo yao.

Kuwafunza wavulana kuwa wawajibikaji (Mkakati Maalumu wa kuwafikia Watoto wa Kiume)

Kwa kuzingatia umuhimu wa Usawa, Mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kaskazini Mashariki unatambua umuhimu wa kuelimisha na kuwawezesha wavulana balehe na vijana wa kiume. Katika Afua ya kwanza ya programu ya ‘DREAMS’, kupitia programu ya ‘Coaching Boys Into Men (CBIM)’ iliyoanzishwa na shirika la FUTURES Without Violence, mradi umelenga kuelimisha na kuhamasisha vijana balehe walioko shuleni kupitia michezo kuwa wenye kuwajibika vyema katika jamii. Vijana wanajifunza kuheshimu Utu, matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii, kuzingatia haki za binadamu na kujenga mahusiano yenye afya. Kupitia ‘CBIM’ jumla wa wavulana 7,750 wame¬fikiwa na kupokea mafunzo haya katika Halmashauri ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza.

Afua ya pili ya utekelezaji wa programu ya kuzuia maambukizi ya VVU na viten¬do vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto (Enabling DREAMS)

Kama Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa yanavyolenga Kutokumuacha mtu yeyote nyuma ‘leave no one behind’, katika kuendelea kuboresha elimu, afya, ulinzi na Ustawi wa wato¬to, Mradi kwa kushirikiana na Taasisi ya ELimu Tanzania (TET), Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji iliandaa mtaala maalumu wa kuongoza elimu ya afya ya uzazi kwa wanafunzi wa kike na kiume katika shule za Msingi na Sekondari.

Wanafunzi hawa ni wenye umri wa miaka 15-17, kupitia program hii ya ‘DREAMS’ inawezesha wasichana na wavulana balehe kupata elimu ya stadi za maisha kuhusu afya ya uzazi, VVU/ UKIMWI na kuzuia ukatili wa kijinsia. vijana hawa wanajifunza kuhusu miili yao, jinsi ya na hatua za kuchukua ili kujikinga na maambukizi ya VVU na ukatili. Hii inasaidia kuwezesha watoto na vijana balehe kubaki shuleni, kuzuia maambukizi ya VVU, kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia nakupunguza mimba za utotoni. Hadi Juni 2024, afua hii ya ‘DREAMS’ imefikia jumla ya vijana wasichana 4,495 na wavulana 2,900

Kupitia afua hizi, jumla ya walimu 330 wamejengewa uwezo katika shule 143 zilizopo katika Halmashauri 8 za Mkoa wa Mwanza. Halmashauri hizo ni Nyamagana, Magu, Misungwi, Sengerema, Buchosa, Ukerewe, Kwimba, na Ilemela.Walimu waliojengewa uwezo huendesha na kusimamia utoaji wa elimu kwa kuzingatia mtaala maalumu ulioidhinishwa na Serikali.

Afua hizi ni sehemu ya kazi zinazotekelezwa na Mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kaskazini Mashariki uliojikita katika kuhudumia watoto walio katika mazingira hatarishi. Kupitia afua na mikakati mingine ya kui-marisha Afya, Elimu, Ulinzi na Ustawi wa mtoto. Mradi umefikia jumla ya watoto 95,074 walio katika mazingira hatarishi. Kati ya hao jumla ya Watoto 94,372 wamefikiwa na huduma za upimaji VVU, jumla ya watoto 89,806 wamepata huduma za lishe na jumla ya watoto 100 wamepata rufaa za huduma kutokana vitendo vya ukatili.

Mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kaskazini Mashariki kupitia programu ya DREAMS, unalenga kuhakikisha watoto wa Tanzania wanapata elimu bora na huduma muhimu zinazosaidia kuboresha maisha yao na kuwalinda dhidi ya hatari mbalimbali ikiwemo maambukizi ya VVU, vitendo vya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.

Tunapoadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, ni muhimu kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali na kuhakikisha watoto wanapata maarifa, maadili na stadi za kazi zinazowaweze¬sha Taifa kuwa na kizazi hodari.

Vailet Mollel ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mradi, Theresia Christian ni Mkurugenzi Mshiriki wa Mawasiliano na Mahusiano ya Nje wa Mradi.


Imeandikwa na Vailet Mollel na Theresia Christian.