Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Malawi, Hayati Saulos Klaus Chilima. Ibada ya Mazishi hayo imefanyika leo Jumapili, Juni 16, 2024 katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi.