SMZ kugharamia mazishi ya wote walioangukiwa na Jumba la Maajabu

Wananchi wakiangalia sehemu ya jengo la kihistoria la Beit-Al-Ajab ambayo iliyobomoka katika eneo la Mji Mkongwe mjini Unguja, Zanzibar jana.

Muktasari:

Serikali imeahidi kugharamia mazi-shi ya watu wawili waliofariki baada ya kudondokewa na jen-go maarufu la kitalii, Beit Al Ajaib (Jumba la Maajabu) lili-lopo eneo la Mji Mkongwe mjini Unguja visiwani Zanzibar.

Dar es Salaam/Unguja. Serikali imeahidi kugharamia mazi-shi ya watu wawili waliofariki baada ya kudondokewa na jen-go maarufu la kitalii, Beit Al Ajaib (Jumba la Maajabu) lili-lopo eneo la Mji Mkongwe mjini Unguja visiwani Zanzibar.

Waliofariki ni Pande Haji Makame (39) na Burhani Ameir Makuno (34) walibainika kati ya saa sita na saa nane usiku kwenye jitihada za kuwatafuta waliofunikwa na kifusi cha jen-go hilo.

Wakati wawili hao waki-tolewa katika kifusi, wengine wanne walikuwa wakitib iwa majereha waliyoyapata katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.

Jumba hilo maarufu lililod-umu kwa zaidi ya miaka 130 lilidondoka juzi mchana na kuwafunika mafundi waliokuwa wakilikarabati.Jana Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla akifuatana na mawa-ziri, wakuu wa mikoa na wilaya aliwatembelea majeruhi wali-olazwa na kwenda eneo la tukio.

Naibu kamishna wa kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar, kamanda Gora Haji Gora alim-weleza Abdulla kwamba uokoaji kufanyika kwa tahadhari kubwa kutokana na mazingira ya tukio lilivyokuwa.

 Kamanda Gora alisema operesheni ya kuondoa kifusi cha jengo hilo itaendelea ili kubaini kama kuna watu wen-gine waliofunikwa.Alipofika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kuwaangalia majeruhi wa ajali hiyo, Abdulla

 alipewa maelezo ya hali zao.Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmo-ja, Dk Marijani Msafiri alim-weleza Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar kwamba maje-ruhi wanaendelea na matiba-bu pamoja na na watafanyiwa uchunguzi zaidi.

Dk Marijani alisema wagon-jwa wawili kati ya wanne wame-fanyiwa upasuaji mguuni kuto-kana na kuangukiwa na kifusi cha jengo hilo. Suleiman aliwa-pa pole wajenzi hao na kuahidi Serikali itahakikisha wanaende-lea kupata huduma zote hadi wataalamu wa afya watakapot-hibitibisha wamepona.Makamu wa Kwanza wa Rais

 wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad naye alitembelea hospi-tali ya Mnazi Mmoja walikolaz-wa majeruhi na kuahidi mbali na kugharamia mazishi ya waliofari-ki, Serikali pia itatoa ubani (ram-birambi).

“Nichukue nafasi hii kuwashu-kuru madaktari, wauguzi na wafanyakazi wote kwa jinsi walivyowashughulikia wagonjwa.“Kwa wagonjwa hawa, nimerid-hika kuwa wanaangaliwa vizuri, pale ambapo itabidi tupate msaa-da kwa ajili ya wenzetu kutoka Dar es Salaam tutafanya hivyo na wako tayari,” alisema Maalim Seif ambaye ni mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo.Katika hatua nyingine, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa haraka ili kubaini chanzo cha kuporomoka kwa sehemu ya jengo la makumbusho la Taifa la Beit al Ajab.

Dk Mwinyi ametoa agizo hilo jana alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja ili kutoa rambirambi kwa wafiwa na kuwa-pa pole majeruhi wa ajali hiyo.Amevitaka vyombo hivyo kufan-ya uchunguzi wa kina haraka ili kubaini chanzo cha kuporomoka kwa jengo hilo na kuleta maafa kwa wananchi ili Serikali ichukue hatua mara moja.

Awali jana, Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar ili-toa taarifa ikieleza imeunda tume maalum kuchunguza chanzo cha kuporomoka kwa jengo la Beit Al Ajaib na kuishauri Serikali hatua zinazostahili kuchukuliwa.

Akizungumza kwa simu na gaze-ti hili, kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadh Juma alisema uokoaji wa waliofukiwa na kifusi unaendelea.

“Pande Haji Makame ni mkazi wa Babwini, Kaskazini Unguja ali-patikana saa sita usiku akioneka-na kujeruhiwa maeneo ya kifua na kichwani na Burhani Ameir Makuno ni mkazi wa Mtoni Kidatu alipatikana saa nane usiku. Miili yote ilipelekwa Hospitali ya Mnazi Mmoja. Tunaendelea kuchukua tahadhari wakati tukifanya kazi hii,” alisema Juma.

Wataalamu wa historia ya Zanzi-bar wanasema jumba hilo la maa-jabu ni maarufu duniani kote kuto-kana na mambo matatu ambayo yamelifanya kuwa na rekodi ya aina yake na kuwa miongoni mwa vivutio vya utalii visiwani hapa.

Jengo la Beit Al Ajaib linashikilia rekodi ya kuwa nyumba ya kwan-za ukanda wa Afrika Mashariki kuwekewa umeme, lifti na bomba la maji ndani. Miundombinu hiyo iliwekwa wakati kwingine kote kukiwa nyuma kimaendeleo.

Habari hii imeandaliwa na Haji Mtumwa na Aurea Simtowe