Sengerema yapoteza Sh61 milioni kusuasua ujenzi wa vibanda

Baraza la madiwani la Halmashauri ya Buchosa wakiwa kwenye kikao Cha mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali CAG. Picha na Daniel makaka

Muktasari:

  • Diwani Sospitar Busumabu amesisitiza umuhimu wa kukamilisha ujenzi huo ili kuongeza mapato

Sengerema. Halmashuri ya Sengerema inapoteza zaidi ya Sh61milioini kila mwaka kutokana na kutokukamilika kwa ujenzi wa vibanda ya stendi kuu ya mabasi iliyoko Bukala mjini Sengerema kutokukamilika.

Hiyo ni moja ya hoja tano zinazowasilishwa  na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenye kikao cha baraza la madiwani la Halmashauri ya Sengerema.

Diwani wa Tabaruka, Sospitar Busumabu amesema halmashauri inatakiwa kuongeza nguzu za kusimamia ujenzi wa vibanda hivyo ukamilike, ili iweze kukusanya mapato na kuhudumia wananchi.

"Hoja hii isingeweza kujadiliwa kama viongozi wa halmashauri wangeweka mkazo wa kuhamasisha vibanda hivi vikamilike na kuanza kutumika,” amesema.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Binuru Shekideke amesema amepokea maoni ya mkaguzi na atahakikisha vibanda hivyo vinajengwa na kukamilika, ili viipatie mapato halmashauri.


Kwa upande wake, Katibu Tawala   Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana ameitaka Halmashauri ya Sengerema kusimamia ujenzi wa vibanda hivyo, ili vikamilike na kuleta manufaa ya kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema, Yanga Malaga amesema atasimamia maelekezo yote yaliyotokewa na CAG kwa Halmashauri ya Sengerema.