Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

92 wafa sababu ya kuharibika kwa mimba

Muktasari:

  • Serikali imesema suala la mimba zisizotarajiwa bado ni tatizo nchini hivyo wananchi na viongozi wanatakiwa kuendelea kutoa elimu kwa wahusika ili kulikomesha.

Dodoma. Katika kipindi cha mwaka 2022 hadi 2024 jumla ya wanawake 92 walipoteza maisha kutokana na changamoto mbalimbali zilizosababishwa na kuharibika kwa mimba, Bunge limeelezwa leo Januari 31, 2025.

Naibu Waziri wa Afya ametoa takwimu hizo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Fatuma Toufiq aliyeuliza ni watoto wa kike wangapi na wanawake wangapi walioathirika na utoaji mimba usio salama nchini.

Ingawa hakueleza kama kuna uhusiano wa moja kwa moja na utoaji mimba, Dk Mollel amesema katika kipindi cha mwaka 2024 wapo wanawake na wasichana waliopata changamoto ya kuharibikiwa na mimba na kupata huduma katika vituo vya huduma za afya.

“Wanawake na wasichana 181,071 ambao walipatiwa huduma na kuruhusiwa kama wagonjwa wa nje (outpatients) na wanawake na wasichana 32,512 walipatiwa huduma wakiwa wamelazwa (inpatients),” amesema Dk Mollel.

Dk Mollel amesema kuendelea kwa tatizo la mimba zisizotarajiwa sio sheria, hivyo kila mmoja asimame kwa nafasi yake kuendelea kupaza sauti kwani bado linawasumbua hata wao katika Serikali.