Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Samatta Uefa ndo basi tena, arudi Europa League

SAMATTAN Pict

Muktasari:

  • Samatta alikuwa anasaka nafasi nyingine ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufanya hivyo na KRC Genk ya Ubelgiji na sasa atacheza Europa League.

KITENDO cha chama la nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, PAOK kushindwa kuingia nafasi mbili za juu kwenye michuano maalumu ya Super League ya Ligi Kuu ya Ugiriki, kimeikosesha tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na sasa imeangukia Europa League.

Samatta alikuwa anasaka nafasi nyingine ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufanya hivyo na KRC Genk ya Ubelgiji na sasa atacheza Europa League.

Katika Ligi Kuu Ugiriki nafasi nne za juu bingwa hapatikani isipokuwa timu nne huanza kushindana upya na inayoshika nafasi ya kwanza na pili zinashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, hukuya tatu na nne zinakwenda kucheza Europe League.

Katika msimamo wa ligi hiyo, PAOK inakamata nafasi ya tatu kabla ya mchezo wa jana dhidi ya AEK Athens na ina pointi 55 baada ya michezo mitano kati ya sita na endapo ikipoteza itamaliza mkiani licha ya kwamba imeshaangukia Europa League.

PAOK katika michezo hiyo, imeshinda tatu na kupoteza mbili, ikishinda mabao 3-2 dhidi ya AEK Athens, 2-1 dhidi ya Olympiacos Piraes na 2-1 dhidi ya Panathinaikos, huku iukipoteza  2-1 dhidi ya Panathinaikos na 4-2 dhidi ya Olympiacos.