Ibraah awasili Basata, Harmonize anasubiriwa

Muktasari:
- Baraza hilo limewataka wasanii hao kufika ofisini hapo leo Jumatatu, saa 2 asubuhi, kutokana na madai ya kulipa Sh1 bilioni aliyoambiwa Ibraah na uongozi wa Lebo ya Konde Gang inayosimamiwa na Harmonize ambaye bado hajafika na anasubiriwa.
MSANII wa Bongo Fleva, Ibrahim Abdallah Nampunga 'Ibraah' tayari amewasili katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) baada ya taarifa za wito kutokana na kile kinachoendelea kati yake na Harmonize.
Baraza hilo limewataka wasanii hao kufika ofisini hapo leo Jumatatu, saa 2 asubuhi, kutokana na madai ya kulipa Sh1 bilioni aliyoambiwa Ibraah na uongozi wa Lebo ya Konde Gang inayosimamiwa na Harmonize ambaye bado hajafika na anasubiriwa.
Uongozi wa Kampuni ya Harmonize Ent. Ltd kupitia Lebo yake ya Konde Gang Music Worldwide ulitangaza kumsimamisha msanii huyo kutoa na kushiriki katika shughuli zozote za muziki kama ilivyoainishwa katika mkataba wake.
katika taarifa ya lebo hiyo, imeeleza pia msanii huyo hatatakiwa kusubiri hadi suala lake litakapopatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa mujibu wa mkataba wake na sheria za Tanzania.
Lebo hiyo pia imemsimamisha kwa sababu msanii huyo kwa madai ya kutoa machapisho yanayomvunjia heshima Harmonize ambaye ndiye bosi wake na kumpiga marufuku kuchapisha, kutamka au kufanya mawasiliano yoyote kuhusu suala hili kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii kama vile Instagram, WhatsApp, Facebook na sehemu nyingine ikiwamo mawasiliano ya aina yoyote ambayo yanaweza kuharibu taswira ya lebo au kumdhalilisha mkurugenzi muwekezaji wa lebo hiyo.