Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeya City yamaliza Championship kibabe, shangwe ikitawala Sokoine

MBEYA Pict

Muktasari:

  • City ikicheza mechi yake ya mwisho msimu huu 2024/25 imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Green Warriors, huku shangwe ikitawala katika uwanja wa Sokoine kwa viongozi , wachezaji na mashabiki kukata keki ya pamoja.

Mbeya City imehitimisha msimu kibabe baada ya kuikanda mabao 5-0 Green Warriors, huku viongozi wa timu hiyo na Chama Cha Soka mkoani humo wakieleza furaha na matarajio yao ya msimu ujao.

Timu hiyo ilishuka daraja misimu miwili nyuma ambapo msimu ujao itacheza tena Ligi Kuu baada ya kumaliza nafasi ya pili kwa pointi 68 ikiachwa tatu na vinara Mtibwa Sugar.

Hata hivyo, kabla ya mechi ya leo kuhitimisha Ligi ya Championship, wachezaji, viongozi na mashabiki waliungana kufanya matebezi ya heshima mitaa mbalimbali ya Jiji la Mbeya kwa lengo la kushukuru wadau kwa sapoti.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, mabao Eliud Ambokile, Rifat Hamis, Malaki Joseph, Willy Thobias na Bruno Shayo.

Akizungumzia matokeo hayo, Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoani hapa (Mrefa), Elias Mwanjala amesema heshima waliyoweka timu hiyo ni ya kupongezwa akiahidi kuwa, Ligi Kuu sasa inaenda kuchangamka jijini Mbeya.

"Tuwapongeze wachezaji, viongozi na wadau wote walioshiriki kuipa sapoti timu hadi kurejesha heshima hii, Mbeya City inayo rekodi zake hivyo msimu ujao furaha inakuja upya," amesema Mwanjala.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoani Songwe (Sorefa), Jacob Mwangosi amesema kupitia soka la Mbeya wamejifunza mengi ambayo yatawasaidia kujijenga.

"Nimekuja kujifunza kitu kupitia Mrefa namna wanavyoendesha mpira, hata kwangu naenda kufanyia kazi namna ya kuhakikisha tunapata timu za ushindani haswa Ligi Kuu," amesema Mwangosi.

Mtendaji Mkuu wa Mbeya City, Ally Nnunduma amesema ni furaha kubwa kuona wanafikia malengo akiwashukuru waliowezesha mafanikio hayo na kwamba msimu ujao yapo mabadiliko makubwa.

"Tutakaa kutathmini wapi tuanzie, kiujumla mafanikio haya si mimi pekee bali wapo wengi wakiwamo Mbunge wa Mbeya Mjini, Meya, Mkurugenzi, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na mashabiki," amesema Nnunduma.