Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipa Mtibwa awapiga mkwara Camara, Diarra

KIPA Pict
KIPA Pict

Muktasari:

  • Malimi amekuwa mhimili mkubwa kwenye mafanikio ya Mtibwa Sugar msimu huu, ambapo timu hiyo imerejea Ligi Kuu Bara ikitwaa ubingwa wa Championship kwa kuvuna alama 71 katika michezo 30.

SAA chache baada ya kuiwezesha Mtibwa Sugar kupanda daraja na kunyakua ubingwa wa Ligi ya Championship, kipa Costantine Malimi amesema kwa sasa ameiva na yuko tayari kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara na kuonyesha ushindani dhidi ya Moussa Camara wa Simba na Djigui Diarra wa Yanga.

Malimi amekuwa mhimili mkubwa kwenye mafanikio ya Mtibwa Sugar msimu huu, ambapo timu hiyo imerejea Ligi Kuu Bara ikitwaa ubingwa wa Championship kwa kuvuna alama 71 katika michezo 30.

Katika ligi hiyo iliyomalizika Mei 11, 2025, Mtibwa imeshinda mechi 22, sare tano na kupoteza tatu, ikifunga mabao 58 na kuruhusu 18.

Malimi amekuwa kinara wa cleensheet (16) na kuiwezesha timu hiyo kuruhusu mabao machache zaidi (18), huku Mbeya City iliyomaliza ya pili na alama zake 68 ikiruhusu mabao 26.

Malimi ambaye ni mchezaji chipukizi aliibuka msimu uliopita katika Ligi Kuu Bara akiwa na Geita Gold ambayo ilishuka daraja na kutimkia Mtibwa Sugar ambayo ameiwezesha kurejea Ligi Kuu Bara na kukiri yuko tayari kuonyesha ubora wake kwenye michuano hiyo mikubwa nchini.

Akizungumza na Mwanaspoti, Malimi amesema matarajio yake ni kupambana na kuonyesha uwezo na ubora wake kila atakapopewa nafasi ili kuendeleza kiwango kizuri alichokionyesha Championship.

“Mchezaji anakuwa yupo tayari muda wote, kikubwa ni kujituma na kujua nini anafanya hii ndiyo kazi yetu kwahiyo hamna utofauti na daraja la kwanza, ni madaraja tu lakini wachezaji ni walewale na mechi ni zile zile,” amesema Malimi.

Ameongeza, kilichombeba ni kuwasikiliza walimu wake na kufanyia kazi huku akiwapongeza mashabiki na kuwaomba wawaunge mkono Ligi Kuu Bara ili kuendeleza moto wao.

“Siri kubwa ni kuwasikiliza walimu wangu na kujua nini nafanya pindi ninapopewa nafasi hicho ndicho kilichonibeba zaidi, nimejisikia faraja na tumefurahi kwa mafanikio haya tuliyoyapata,” amesema Malimi aliyewahi kuidakia Geita Gold ilipokuwa Ligi Kuu kabla ya kushuka msimu uliopita.