Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KMC yamfuta kazi Ongala, mwenendo mbovu wa timu watajwa

Muktasari:

  • Uamuzi huo umefanyika baada ya kocha huyo kuitumikia timu hiyo kwa miezi mitano na siku 21 tu tangu alipochukua mikoba ya Abdi Hamid Moalin ambaye aliachana na timu hiyo na kujiunga na Yanga.

Timu ya KMC ya Kinondoni, Dar es Salaam imeamua kuachana na kocha wake, Kally Ongala kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Uamuzi huo umefanyika baada ya kocha huyo kuitumikia timu hiyo kwa miezi mitano na siku 21 tu tangu alipochukua mikoba ya Abdi Hamid Moalin ambaye aliachana na timu hiyo na kujiunga na Yanga.

Mmoja wa viongozi wa KMC amesema kuwa sababu ya kuachana na Ongala ni timu hiyo kutokuwa na muendelezo wa matokeo mazuri chini yake tangu alipojiunga nayo pamoja na kiwango kisichoridhsha,

"Ni kweli tumeamua kuvunja mkataba wa kocha Ongala na sababu ni mwenendo usiorisha wa timu kwa maana ya matokeo lakini pia hata namna inavyocheza ni vibaya jambo linalosababisha ipoteze pointi kirahisi kwenye mechi nyingi," amefichua kiongozi huyo.

Katika kipindi cha miezi mitano aliyosimamia benchi la ufundi la KMC, timu hiyo imecheza mechi 15 za Ligi Kuu ambapo imekusanya pointi 16 tu jambo lililochangia kwa kiasi kikubwa iwe katika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu msimu huu.

Baada ya uongozi wa KMC kuvunja mkataba na Kally Ongala, jukumu la kusimamia benchi la ufundi la timu hiyo katika mechi nne ilizobakiza za Ligi Kuu imeliacha kwa kocha wa viungo, Adam Mbwana.