Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AKILI ZA KIJIWENI: Pawasa kafanikiwa bado Aggrey Morris

PAWASA Pict

Muktasari:

  • Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ ilikuwa Morocco ambako ilikuwa inashiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo (AFCON U17) zilizofanyika huko Morocco ambako iliishia hatua ya makundi.

HAPA kijiweni tumefuatilia kwa ukaribu muenendo wa timu zetu mbili tofauti za vijana za wanaume ambazo zilikuwa na kibarua cha kushiriki mashindano ya umri wao yanayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ ilikuwa Morocco ambako ilikuwa inashiriki Fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo (AFCON U17) zilizofanyika huko Morocco ambako iliishia hatua ya makundi.

Serengeti Boys kwenye mashindano hayo ilinolewa na beki wa zamani wa Azam FC na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Aggrey Morris.

Baada ya hapo timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ikashiriki fainali za soka za shule Afrika na ikatwaa ubingwa ambao ulikuwa wa pili kwake mfululizo baada ya kutwaa kwa mara ya kwanza wakati fainali hizo zilipofanyika Zanzibar.

Hii timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 ambayo imeshiriki fainali za Afrika za shule na kutwaa taji iliongozwa na beki wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Boniface Pawasa.

Kwa Pawasa kuchukua taji hilo, amethibitisha namna ambavyo amekuwa kocha mzuri wa soka kwa vile alikuwa msaidizi wakati timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ inatwaa ubingwa wa mashindano ya CECAFA mwaka 2019 kule Uganda.

Baadaye akaiongoza timu ya taifa ya soka la ufukweni kufuzu fainali za mataifa ya Afrika na leo hii kaonyesha makali yake kwa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 15 ambayo imeondoka kwa heshima kule Ghana.

Kwa Aggrey Morris labda inawezekana mambo hayajamuendea vizuri katika fainali za AFCON U20 kwa vile ndio mashindano ya kwanza makubwa kwake kuiongoza timu akiwa kocha mkuu hivyo kukosa uzoefu kunaweza kukawa kumemuangusha.

Natamani Aggrey Morris apewe tena fursa nyingine siku za usoni tuone kama hilo la kukosa uzoefu ndio kweli limemkwamisha au bado anahitajika kurudi upya msituni kujipanga ili aingie katika daraja la mwenzake Pawasa.