Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zimamoto, Uhamiaji zashindwa kutambiana

ZIMAMOTO Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo ilikuwa ni ya raundi ya 23 baada ya kusimama kupisha michuano ya Kombe la Muungano, ambapo Zimamoto ilitolewa nisu fainali kwa kufungwa na Yanga kwa penalti baada ya dakika 90 kuisha kwa sare ya 1-1.

LIGI Kuu ya Zanzibar, imerejea tena jioni ya leo Ijumaa, ikishuhudiwa timu za Zimamoto na Uhamiaji zikishindwa kutambiana kwa kutoka sare ya 1-1 katika mechi kali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mao Zedong, mjini Unguja. 

Mechi hiyo ilikuwa ni ya raundi ya 23 baada ya kusimama kupisha michuano ya Kombe la Muungano, ambapo Zimamoto ilitolewa nisu fainali kwa kufungwa na Yanga kwa penalti baada ya dakika 90 kuisha kwa sare ya 1-1.

Dakika 45 za kwanza za mechi hiyo ziliishankwa suluhu licha ya timu zote kushambuliana kwa zamu kusaka mabao.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na dakika ya 62  Abdulhamid Ramadhan aliitanguliza Zimamoto kwa bao safi, kabla Yahya  Haji Salmini kuisawazishia Uhamiaji katika dakika ya 70 kwa mkwaju wa penalti.

Licha ya sare hiyo, lakini Zimamoto ilionekana kutengeneza nafasi nyingi za kupeleka mashambulizi kwa Uhamiaji kwa muda mrefu, ila umakini mdogo uliwaangusha.

Katika mchezo mwingine wa Ligi hiyo uliopigwa pia jioni  hii  KVZ ilipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Inter Zanzibar na kuzidi kuiweka pabaya, timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu, kwani imebakia na pointi tano ikiwa nafasi ya pili toka mkiani.

Ligi hiyo itaendelea kesho Jumamosi kwa mechi mbili, mjini Unguja kwenye Uwanja wa Mao A, vinara Mwembe Makumbi itapepetana na Mlandege iliyopo nafasi ya pili, ilihali kisiwani Pemba, Chipukizi na Mwenge zitaumana kwenye Uwanja wa Gombani.