Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rose Muhando amuombea Harmonize aoe

ROSE Pict

Muktasari:

  • Dua hiyo imekuja baada ya Harmonize kucheza challenge ya wimbo wa Rose Muhando uitwao ‘Amina’ na kwa kitendo hicho Rose amesema kimempa heshima kubwa kwake na kujua ni shabiki wa kazi zake.

MKONGWE wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando amesema amekuwa akimuombea dua njema mkali wa Bongo Fleva, Harmonize a.k.a Konde Boy, ili aweze kuzidi kufanikiwa katika kazi zake za sanaa na kubwa zaidi aoe mwaka huu.

Dua hiyo imekuja baada ya Harmonize kucheza challenge ya wimbo wa Rose Muhando uitwao ‘Amina’ na kwa kitendo hicho Rose amesema kimempa heshima kubwa kwake na kujua ni shabiki wa kazi zake.

Rose  alisema atazidi kumuombea dua njema, Harmonize ili aweze kupata mwanamke mwema mwaka huu wa kumuoa.

“Kiukweli nitoe pongezi kwa Harmonize kwa kuweza kucheza chalenji ya wimbo wangu wa Amina, kitendo hiki ni kikubwa sana kwangu kwani ni wasanii wachache wakubwa wenye kuweza kusapoti kazi za watu wengi kama hivyo, na napenda pia kuona kijana huyu (Harmonize) mwaka huu apate mke mwema wa familia na kuoa kabisa. Hii dua naiomba kuanzia sasa,” alisema Rose.

Chalenji ya kucheza wimbo wa Amina uliotoka 2009, imeibuliwa upya kwa kasi sana katika mtandao wa TikTok hivi karibuni kwa baadhi ya watu kucheza na kuanguka.