Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mayele: Bidhaa ya Ligi Kuu inayotikisa soko Misri

MAYELE Pict

Muktasari:

  • Mwamba huyu ni bidhaa iliyofanya vizuri katika Ligi Kuu Bara ndani ya misimu miwili akiwa na Yanga, na sasa inasumbua zaidi Misri, ligi namba moja kwa ubora barani Afrika.

STRAIKA wa mabao Fiston Mayele ameendelea kuthibitisha kuwa mmoja wa washambuliaji bora zaidi katika bara hili kwa sasa akiwasha moto katika Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu ya Misri akiwa na Pyramids.

Mwamba huyu ni bidhaa iliyofanya vizuri katika Ligi Kuu Bara ndani ya misimu miwili akiwa na Yanga, na sasa inasumbua zaidi Misri, ligi namba moja kwa ubora barani Afrika.


FAINALI CAF

Mabao mawili aliyofunga katika nusu fainali dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini yamemfanya Mayele afikishe mabao matano na kuwa kinara sawa na Emam Ashour wa Ahly na Ibrahim Adel wa Pyramids.

Mabao hayo yamechangia kuipeleka timu yake katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Pyramids itacheza na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini.

Hii ni fainali ya pili kwa Mayele kwenye mashindano ya CAF baada ya ile ya msimu 2022/23 akiwa na Yanga alipoibuka mfungaji bora kwa mabao 7.

MAYE 01

Rekodi zake kimataifa Mayele amecheza jumla ya mechi nane (dakika 682) akifunga mabao matano katika mashuti 16 aliyopiga.


ANACHOKIFANYA MISRI

Kwenye msimu wake wa kwanza 2023/24 alicheza mechi 32 za mashindano yote na kufunga mabao 17 na asisti tano.

Licha ya ugeni wa ligi hiyo lakini namba zilionekana kumbeba Mayele kwenye msimu wake wa kwanza tu.

Akiendelea kupewa nafasi ndani ya kikosi hicho kilichosheheni nyota kibao msimu huu tayari amefunga mabao sita na asisti mbili kwenye mechi 19 za Ligi Kuu.

MAYE 02

YANGA

Mayele aliitumikia Yanga kwa misimu miwili akijiunga nayo msimu wa 2021/2022 akitokea AS Vita ya kwao DR Congo.

Nyota huyo alikuwa mhimili mkubwa wa Yanga na kwenye safu ya ushambuliaji ya timu hiyo katika michuano yote ile ya Ligi Kuu na mashindano ya CAF.

Katika msimu wa kwanza, staa huyo aliyesifika kwa staili yake ya kushangilia kwa ‘kutetema’, alishika namba mbili kwenye vinara wa upachikaji wa mabao wa Ligi Kuu akifunga mabao 16, nyuma ya kinara George Mpole aliyeifungia Geita Gold aliyemaliza mabao 17.

Hakuishia hapo, alifunga mabao mawili katika Kombe la Shirikisho (ASFC), na msimu huo huo alifunga bao moja kwenye mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa jadi Simba.

MAYE 03

Kiufupi katika msimu wa 2021/22, Mayele alifunga jumla ya mabao 19 katika Ligi Kuu, ASFC na Ngao ya Jamii.

Msimu uliofuata akafunga mabao 17 na kuibuka mfungaji bora sawa na rafiki yake wa karibu Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ aliyekiwasha Simba.

Akatwaa tuzo ya kibao ikiwamo Mchezaji Bora wa msimu sambamba na Bao Bora na pia alitajwa kwenye kikosi cha msimu cha Ligi Kuu 2022-23.

Msimu huo ndio aliisaidia Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika akiibuka mfungaji bora wa michuano hiyo akifunga jumla ya mabao saba akifuatiwa na Rango Chivaviro wa Marumo Gallants aliyefunga sita.

MAYE 04

Ikumbukwe pia kabla ya kudondokea katika Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga ilianzia kwenye Ligi ya Mabingwa na huko Mayele alifunga mabao saba akipiga hat-trick mbili dhidi ya Zalan FC ya Sudan na bao moja dhidi ya Al Hilal katika sare ya mabao 1-1, nyumbani kwa Mkapa kabla ya kutolewa kwa kuchapwa 1-0 ugenini pale Omdurman, Sudan.

Pia aliitungua Simba mabao mawili katika mchezo wa Ngao ya Jamii msimu huo, mechi iliyomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-1 na pia kwenye ASFC ambako Yanga iliitwaa taji hilo akifunga mabao mawili.

Kiufupi msimu huo Mayele alifunga jumla ya mabao 35, kwenye Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Afrika, Kombe la Shirikisho Afrika,  ASFC na Ngao ya Jamii.

Kwa maana hiyo katika misimu miwili ambayo Mayele alicheza Yanga alifunga jumla ya mabao 54, rekodi ambayo inambeba hadi leo.

Baada ya kucheza kwa mafanikio makubwa Yanga nyota huyo akatimkia Pyramids ambako sasa anajiandaa kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Matarajio ya baadhi ya mashabiki ilikuwa atashindwa kuonyesha ubora Misri katika ligi namba moja kwa ubora barani humu.

MAYE 05

Hilo linatokana na rekodi ya baadhi ya mastaa ambao walifanya vizuri nchini lakini walipouzwa nje hawakuonyesha kiwango bora wakishindwa kuendana na kasi ya ligi hizo.

Miongoni mwa nyota hao ni Clatous Chama wakati anacheza Simba aliuzwa kwenda RS Berkane ya Morocco hakuonyesha kiwango bora na baadaye akarejea unyamani.

Mwingine Luis Miquissone aling’ara Simba, alipouzwa Al Ahly (Misri), alikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara baadaye akarejea tena Simba.