Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni zama za utawala wa Arsenal

ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Mafanikio hayo yanakamilisha mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Kocha Mikel Arteta ndani ya klabu hiyo karibu miaka saba, huku sasa akichukua hatua kubwa zaidi za kuifanya kuanza utawala mpya wa soka nchini humo.

LONDON, ENGLAND: Imesubiri kwa muda mrefu, hatimaye baada ya miaka 22, Arsenal imetwaa tena ubingwa wa Ligi Kuu ya England.

Mafanikio hayo yanakamilisha mabadiliko makubwa yaliyofanywa na Kocha Mikel Arteta ndani ya klabu hiyo karibu miaka saba, huku sasa akichukua hatua kubwa zaidi za kuifanya kuanza utawala mpya wa soka nchini humo.

Kikosi chake kimeondoa sifa ya kuwa “wanaokaribia, lakini hawafiki” baada ya kumaliza nafasi ya pili mara tatu mfululizo, na sasa baada ya ukame wa mataji kumalizika, mawazo yanaweza kuelekezwa kwenye siku zijazo.

“Hiyo ilikuwa ya kupendeza,” amesema Arteta baada ya kuinua kombe la Ligi Kuu kwa mara ya kwanza, akiliinua juu kwenye Uwanja wa Selhurst Park kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace Jumapili.

ARSN 01

“Angalia furaha ya watu wote, wamekuwa wakingojea hili kwa muda mrefu sana. Tumepitia nyakati ngumu njiani, lakini yote yalikuwa na thamani unapoona mwitikio wa aina hii.

“Sasa ni wakati wa kufurahia na kuvua kofia ya ukocha.

“Nadhani tulionesha mshikamano wa ajabu, kujitoa na ujasiri. Kila kitu kilichotuzunguka kiliongeza hamasa yetu ya kufanya hivi.” Huku wakijiandaa na fainali ya Ligi ya Mabingwa UEFA  dhidi ya Paris Saint-Germain itakayochezwa Jumamosi, huu unaweza kuwa mwanzo wa kipindi cha utawala wa kweli kwa Arsenal.


Ni kipindi cha utawala?

Sababu kubwa inayoufanya ubingwa huu kuwa hatua muhimu ya kisaikolojia kwa Arteta na Arsenal ni kwamba kocha huyo ameweza kumshinda rafiki yake wa muda mrefu na mwalimu wake, Pep Guardiola.

ARSN 02

Kocha huyo wa Manchester City, ambaye anaondoka baada ya misimu 10, ndiye aliyekuwa sababu ya maumivu mengi ya Arsenal katika miaka ya karibuni. Sasa Arteta akimshinda mwenzake wa zamani, muda wa mafanikio ya kudumu unaweza kuwa umefika. Wapinzani wa msimu uliopita, Liverpool, walimaliza nyuma ya Arsenal kwa tofauti ya pointi 25, huku kukiwa na mjadala kuhusu kama Arne Slot ndiye mtu sahihi wa kuwarudisha kwenye ushindani wa ubingwa.

Manchester United, licha ya kuimarika chini ya Michael Carrick, bado hawajarejea kuwa wapinzani wa mara kwa mara, huku Chelsea wakiwa na msimu wa kukatisha tamaa na kumaliza katikati ya msimamo. Arteta tayari amebadili ujumbe kwa wachezaji wake kuhusu jinsi fikra zao zitakavyobadilika sasa kwa kuwa wao ni mabingwa wa ligi, huku akiwataka kuongeza mataji zaidi.

ARSN 03

Kwa nini Arsenal wanaweza kwenda hatua inayofuata

Arteta tayari amesema anataka “kuwa na gwaride la mataji mawili makubwa” akilenga kushinda Ligi ya Mabingwa UEFA kwa mara ya kwanza katika historia ya Arsenal.

Arsenal walimuunga mkono Arteta kwa kutumia takribani pauni 250 milioni majira ya joto yaliyopita kuongeza ubora na kina cha kikosi. Arteta anataka kujenga urithi wa mafanikio ya kudumu kwa Arsenal, na baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa, mwelekeo utakuwa kumpa mkataba mpya.