Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hawa wameoga tu, mjini hawaendi

WAMEOGA Pict

Muktasari:

  • Medali za ubingwa huwa zinatolewa kwa wachezaji, makocha na maofisa wa klabu kwa vile ambavyo timu itaona inafaa.

LIVERPOOL, ENGLAND: BAADA ya kutangazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu England jana, moja kati ya mtihani mwingine ambao unawakabili Liverpool kwa sasa ni kuamua nani atavaa medali na nani hatovaa.

Medali za ubingwa huwa zinatolewa kwa wachezaji, makocha na maofisa wa klabu kwa vile ambavyo timu itaona inafaa.

Kwa mujibu wa kanuni, jumla ya medali 40 za fedha zitatolewa kwa Liverpool ambapo kwa upande wa wachezaji, wale wote ambao wamecheza walau mechi za EPL msimu huu watakuwa na haki ya kuzivaa.

Hadi kufikia sasa, Liverpool ina wachezaji 21 wa kikosi cha kwanza ambao wametimiza kigezo hicho na watatakiwa kuwekwa katika hasabu, hivyo medali zilizobaki ni 19 tu.

Kuna orodha ya wachezaji ambao huenda wameshangilia bure tu ubingwa na inawezekana wasivae kabisa medali za ubingwa kwa sababu idadi ya mechi walizocheza hazifiki tano.

Federico Chiesa ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao hawajacheza mechi tano ingawa bado ana nafasi ya kukamilisha idadi hiyo katika mechi zilizosalia.

Hata hivyo, kuna uwezekano pia wa medali kuongezwa kuwa zaidi ya 40, lakini ni kwa kutuma maombi kwenda bodi ya ligi na sharti lazima kuwe na wachezaji zaidi ya 39 ambao wamecheza mechi tano na zaidi za EPL.

Vitezslav Jaros na Jayden Danns ni miongoni mwa wachezaji wengine ambao hawajakidhi vigezo vya kupata medali.

Tyler Morton alijumuishwa katika kikosi cha EPL mwanzoni mwa msimu huu, lakini hajatimiza vigezo kwani licha ya kucheza mechi tano zote zilikuwa za Kombe la Carabao na FA.

James McConnell na Trey Nyoni pia ni wachezaji wengine ambao hawajatimiza vigezo.

Wachezaji waliotimiza vigezo:

Alisson Becker, Caoimhin Kelleher, Virgil van Dijk, Ibrahima Konate, Joe Gomez, Trent Alexander-Arnold, Andy Robertson, Kostas Tsimikas, Jarell Quansah, Alexis Mac Allister, Curtis Jones, Ryan Gravenberch, Dominik Szoboszlai, Wataru Endo, Harvey Elliott, Mo Salah, Luis Diaz, Diogo Jota, Darwin Nunez, Cody Gakpo.